Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae akizungumza na waandishi wa habari kuhusu na
Kundi la Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
Mnyama Ngiri akiwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan akila majani
Mamba akiwa pembezoni mwa Mto Wami uliopita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan
Mnyama Twiga akila majani kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama walivyokutwa
Watalii kutoka maeneo mbalimbali dunia wakiwa wameshuka kwenye magari ya Utalii tayari kupanda ndege kuelekea Visiwani Zanzibar baada ya kumaliza kutalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan
              

Watalii kutoka maeneo mbalimbali dunia wakiwa kwenye magari ya wazi wakitalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan

HIFADHI ya Taifa ya Saadani imesifu juhudu kubwa zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli kuendeleza sekta ya Utalii hapa nchini kutokana na uwekezaji wa usafiri wa anga ambao umewawezesha watalii kufika moja kwa moja nchini.

Hatua hiyo imesaidia sana kuimarika kwa utalii hapa nchini kutoka mataifa mengine kutokana kwenye nchi zao na kuweza kuja moja kwa moja Tanzania.


Hayo yalisemwa na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo ambapo pia alisema serikali ya awamu ya tano imefanya kazi kubwa ya uboreshaji miundombinu.

Ambapo alisema hilo limesaidia ongezeko la watalii kutokana na wageni wengi kuthamini sana muda ambapo sasa wageni wanaau wezo wa kwenda mahali popote bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote.

Hata hivyo Afisa Utalii huyo alisema pia suala jambo jingine ambalo limefanywa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt Magufuli na kuwa na tija kubwa kwao kuitendaji ni mabadiliko ya mfumo wa kutoka kwenye kufanya kazi kiraia kwenda Jeshi Usu.

“Kwani kwenye Hifadhi za Taifa Tanzania ni muhimu katika suala la ulinzi na uhifadhi kwa sababu imeleta ukakamavu na hari ya mbinu za kivita kuweza kukabiliana na majangili”Alisema Mbae.


Alisema kwani majangili hao wamekuwa ni nia mbaya ya kuihujumu serikali kwenye hifadhi hivyo uwepo wa mfumo huo umesaidia kupunguza changamoto za namna hiyo na kuwawezesha wanyama kuzidi kuongeza kwenye hifadhi.

Akizungumzia mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa eletroniki kwa njia ya mtandao umekuwa ni muhimu sana kwao kwani mepunguza viatarishi kutokana na watu kubeba fedha zao mkononi na wanapofika getini wanalipa.

“Lakini kwa sasa hauihitaji kutembea na fedha kwenye mkoba bali unalipa kwa mfumo wa mtandao ambao umerahisisha wageni wanapoingia kutokana na viatarishi vya kubeba pesa taslimu mkononi”Alisema
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: