Friday, 21 February 2020

HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA YATOA MAFUNZO KWA VIKUNDI

Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Iringa akitoa mafunzo kwa vikundi vya wanawake mjini Iringa leo 
Baadhi ya wanavikundi wakiwa katika mafunzo 

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia Ofisi ya Maendeleo ya Jamii imetoa semina ya mafunzo kwa vikundi 48 vya wanawake na vijana kwa lengo kuwasaidia kujiendeleza katika biashara zao mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Well Faire mwandishi Sima Bingileki anaripoti .

Aidha katika mafunzo hayo, mada mbalimbali zimeweza kuwasilishwa na Maafisa Maendeleo wa Manispaa ikiwa ni pamoja na Elimu ya vikundi, Ukimwi na Vigezo vya upatiwaji wa Mikopo itakayotolewa kwao mara baada ya kukamilika kwa ujazaji wa mikataba waliopatiwa.

"Ama kweli tumefurahishwa na mafunzo tuliyopatiwa na tunaamini mikopo tutakayo patiwa itatunufaisha katika biashara zetu na kutufanya kusimama imara na kuzisaidia Familia zetu" Zainabu Nyan'gole alizungumza hayo akiwa ni mmoja wa waliohudhuria katika mafunzo hayo.

No comments:

Post a comment