Wednesday, 19 February 2020

DC MOFUGA AFANYA MAAMUZI MAGUMU MGOGORO WA JENGO MBULU

Mkuu wa wilaya ya Mbulu  Chelestino  Mofuga akiwa katika eneo la mgogoro na kamati yake ya ulinzi na usalama
Mkuu wa wilaya ya Mbulu  Chelestino  Mofuga akifunguliwa geti kuingia eneo la mgogoro 

Mkuu wa wilaya ya Mbulu  Chelestino  Mofuga amefanikiwa kutatua mgogoro wa jengo ambalo mfadhili Lilian Ann raia wa Norway  alitapeliwa .


Mofuga alisema mgogoro huo uliodumu kwa muda ulihusu jengo hilo lililojengwa kwa sh milioni 87 pamoja na kuweka  vifaa  kwa ajili ya kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi .

Ambapo  Lilian Ann  alikuwa akituma  fedha hizo kupitia hospitali ya Kilutheri Haydom kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto huku Hospitali ya Haydom ilihamisha fedha hizo kama walivyokubaliana .


Lakini Melkizedeck Tippe alipokea fedha  hizo na kununua eneo ambalo aliandika jina la CBO yake anayomiliki binafsi badala ya taasisi iliyokuwa imekubaliwa katika vikao vya maamuzi vya bodi ya wadhamini ambayo ni Haydom Gods children organization .

Alisema mkuu huyo wa wilaya kuwa badala yake aliandika jina la 4Angle disables children programs inayomilikiwa na yeye binafsi .

kabla ya maamuzi kamati ya ulinzi na usalama ilijiridhisha mambo makuu matatu, moja vyanzo vya fedha vilivyotumika kununua na  Kujenga kituo chichi, pili mchakato wa kununua na kupata hati kama ulifuata  sheria ,taratibu na kanuni  na tatu kama bodi ya wadhamini ilishirikishwa kikamilifu katika kila hatua.

Hata hivyo ikibainika kuwepo kwa ukiukwaji wa   mchakato karibu yote na kwamba fedha zote zilitoka kwa mfadhili Lilian Ann.

Hivyo kutokana na kujiridhisha pasipo shaka mkuu huyo  wa wilaya alifanya maamuzi ya kuagiza ukaguzi wa fedha, uchunguzi wa mchakato wa hati na kukabidhi jengo na vifaa vyote kuwa chini ya usimamizi wa mkurugenzi  wa halmashauri  ya wilaya hadi  hatua zote za kisheria zitakapokamilika ili kumrejeshea umiliki wa jengo na vifaa mfadhili kupitia Shirika lake la Haydom Gods children Organization.

No comments:

Post a comment