Friday, 21 February 2020

DC Mofuga achanja bunga kwenda kutatua mgogoro..

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akiongoza kamati ya ulinzi na usalama kwenda kutatua mgogoro wa ardhi 

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akizungumza na wananchi 
Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa kazini 
DC Mofuga akipumzika 
...................

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga
  ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kutembea kilometa 14 kwenda  mpakani mwa kata za Silaloda na Endahagichan ili kuzuia  mapigano ya wananchi wa kata hizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya  wananchi wa kata ya silaloda kuchukua silaha za kijadi na kwenda mpakani kuhamisha mpaka uliwekwa na serikali na kuweka wa kwao kwa ukuta wa  miti.

Akizungumza na wananchi hao Mofuga  amekemea vikali viongozi ambao wanajihusisha  kuchochea uvunjifu wa amani katika eneo hilo na kuwa hatavumiliwa kamwe.

Aidha amewataka  viongozi wote kuzingatia viapo vya maadili na uadilifu wa kulinda rasilimali za nchi, na kulinda amani na utulivu , huku akionya yeyote atakayerudia kufanya hivyo kuwa atachukuliwa hatua Kali zaidi.

"wote waliohusika wametakiwa  kufika ofisini kwangu  na serikali zao kabla ya saa mbili asubuhi kwa kikao zaidi"

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewaasa viongozi kujenga tabia ya kukaa vikao kuongea changamoto za maeneo yao badala kukimbilia kwa mkuu wa wilaya hata migogoro inayoweza kutatiwa na viongozi wa kata na vijiji.

Huku akiwataka   wataalam kwenda kubaini mipaka ya kata hizo na kuwakabidhi wananchi kusimamia.

No comments:

Post a comment