Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga ( katikati), akikabidhi vinywaji kwa Watoto Yatima wa Kituo cha Shalom kilichopo Karatu mkoani Arusha hivi karibuni. Kushoto ni kiongozi wa watoto hao, Frank na wa pili kulia ni Mlezi wa Kituo hicho, Warra Nnko.
 Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga, akiwa na watoto wawili wa kituo hicho.
Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dkt. Donald Kisanga, akiwa na furaha wakati akikabidhi vinywaji kwa watoto wa kituo hicho.
Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania ((TAMUFO) umetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwa watoto Yatima wanao lelewa katika Kituo cha Shalom kilichopo Karatu mkoani  Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Rais wa TAMUFO Dkt.Donald Kisanga alisema msaada huo ulikwenda sanjari na kula chakula pamoja na watoto hao ikiwa ni kusherehekea nao kuukaribisha mwaka mpya wa 2020.
"Sisi kama TAMUFO tuliona katika kusherehekea mwaka mpya tuje tujumuike na watoto hawa kwa kula pamoja nao ili nao wajione kama watoto wengine" alisema Kisanga.
Dkt. Kisanga aliwasa watoto hao kuzingatia masomo kwani ndio urithi wa maisha yao na kuwa  na maadili mema pamoja nakutosahau  kumcha Mungu jambo litakalo waisaidia kuishi vizuri katika Jamii.
Mlezi wa kituo hicho chenye watoto zaidi ya 85, Warra Nnko (Maarufu Mama Shalom) aliushukuru uongozi wa TAMUFO kwa msaada huo pamoja na kujumuika kupata chakula cha pamoja na watoto hao.
"Nitoe shukurani zangu kwa TAMUFO hasa Rais Dkt. Donald Kisanga kwa kuwa jali watoto hawa tunaomba na watu wengine kuiga mfano wenu kwani bado wana mahitaji mengi" alisema Nnko.
Akitoa shukurani kwa niaba ya wenzake kiongozi wa watoto hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Frank aliwashuru TAMUFO kwa kuwapa faraja hiyo na kuomba makundi mengine yajitokeze kuwasaidia badala ya kukuiachia kituo hicho pekee.
Share To:

Post A Comment: