Spika wa Bunge, Job Ndugai Leo Ijumaa Januari 31, 2020 amesema wanamsubiri Mbunge Zitto Kabwe awaeleze kwanini aliandika barua kwa benki ya dunia kuzuia mkopo kwa ajili ya elimu nchini 

Fedha za mkopo huo ambazo ni zaidi ya Sh1.2 Trilioni zingeelekezwa katika programu za shughuli za elimu.

Kikao hicho kilipangwa kufanyika Jumanne Januari 28, 2020  kwa ajili ya kuidhinisha mkopo huo, lakini kikaahirishwa dakika za mwisho kutokana na kile kilichoripotiwa na vyombo vya habari vya nje kuwa ni ombi la taasisi ya kijamii ambayo ina wanachama wake Tanzania.

"Waheshimiwa Wabunge wakati mwingine mwenendo wetu haueleweki, mwenzetu Zitto Kabwe atakaporudi labda atafafanulia wenzake, kuandika barua World Bank kwamba nchi yetu ikose fursa ya mkopo ambao lengo lake ni elimu, nadhani ni kwenda mbali mno na sijui katika hilo unafaidika nini kwa sababu kama ni tofauti za kisera hayo ni mambo ya kujadili tu, hili limetugusa na kutukera wengi" amesema Spika Ndugai na kuongeza;

"Ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Jana, Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora, Joseph Kakunda  ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara  wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendoi), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

 “Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda


Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: