Thursday, 23 January 2020

PWC Yawawezesha Kiuchumi Wanawake Zaidi Ya 100


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Shirika lisilokua la kiserikali la wanawake wafugaji (PWC) limewawezesha wanawake kutoka jamii ya wafugaji zaidi  ya 100 kutoka wilaya  Ngorongoro mkoani Arusha kwa kutoa mikopo na mafunzo mbalimbali ya kujiendeleza kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za ufungaji wa solar,biogas ,ujenzi pamoja ujasiriamali.

Mratibu wa Elimu kutoka shirika hilo Selina Ngurumwa  amesema kuwa mradi huo unaitwa Energizer umefadhiliwa na shirika la Un Women ambao ni wafadhili wakubwa na wanautekeleza kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wakiwemo CAMARTEC ,Mobisol , na Solar Sisters.

Anasema kuwa wanawake wanaofadhiliwa na mradi huo kutoka katika vijiji mbalimbali wametapa mafunzo na kwa sasa wanafanya kazi mbalimbali ikiwemo mkufunga mitambo ya sola katika kaya mbalimbali na pia wanaweza kufanya shughuli za ujenzi.

“Mradi huu ni Mkombozi kwa wanawake waliokosa fursa katika mfumo wa elimu ulio rasmi wanaweza kupata elimu itakayowawezesha kujikwamua na kuondokana na umasikini” Anaeleza Selina

Afisa Maendeleo ya jamii  Mkoa wa Arusha Blandina Nkini amelipongeza shirika hilo kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza ukatili wa kijinsia unaosababishwa na umasikini,utegemezi uliopitiliza pamoja na mila kandamizi.

Blandina anasema kuwa uwezeshaji kiuchumi ni nyenzo muhimu katika kuwakomboa wanawake kutoka katika makucha ya mfumo dume na mila kandamizi zinazochochea ukatili wa kijinsia hivyo wanawake wakiwezeshwa wataweza kujenga familia zao na kuwa na mchango katika jamii.

Mkuu wa Kitengo cha kuwawezesha wanawake  Kutoka Shirika la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya jinsia na wanawake  UN-Women , Lilian  Mwamdanga  amesema kuwa shirika hilo limefanya juhudi za kuwawezesha wanawake wa jamii  ya kifugaji kupitia mradi wa Energizer ambao umewapa nguvu wanawake kutokua tegemezi hivyo kupunguza ukatili

Kwa upande wao wanawake walionufaika na mradi wa kuwawezesha wanawake Nookishon Luka  na Mary Paul ambao hawakupata fursa katika mfumo wa elimu ulio rasmi na wanapatiwa mafunzo maalumu yanawowezesha   kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi uliopitiliza ambao ni kichocheo cha ukatili wa kijinsia.

No comments:

Post a comment