NA HERI SHAABAN

MEYA wa halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amewataka Wanawake wa halmashauri ya Ilala kujikwamua ili kukuza uchumi wa nchi.


Meya Kumbilamoto aliyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya Wanawake na Vijana Wajasiriamali wa Kata ya Gongolamboto yalioandaliwa na taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo.

"Nampongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau, katika juhudi zake za kuisaidia serikali hasa wilayani Ilala kuwainua wanawake katika shughuli za uzalishaji  kwa kuwapatia ujuzi sasa wanamiliki viwanda vyao "alisema Kumbilamboto


Kumbilamoto alisema imefika sasa Wanawake kusimamia imara katika viwanda vidogovidogo ambavyo vinazalisha bidhaa na kuzitangaza katika masoko ya ndani na nje.

Alisema serikali mwaka huu inakabidhia soko la kisasa la Kisutu ambalo ujenzi wake umegharimu bilioni 13   litakapoanza kutumika soko hilo watawekwa wafanyabiashara wa awali na nafasi za Wafanyabiashara 700 zitakuwepo hivyo ameitaka taasisi hiyo na wafanyabiashara kuchangamkia fursa kwani soko hilo litakuwa la kisasa na watalii watafikia hapo ndio mradi mkubwa wa soko la kipekee Ilala

Amewataka wananchi wa Ilala kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kukuza uchumi viwanda 

Alisema serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli inatoa mikopo ambayo aina riba kupitia halmashauri kwa vikundi vinavyotambulika wakopaji wakope fedha hizo na wakumbuke marejesho  ili wengine waweze kukopa .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau amempongeza Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto ambaye ni mlezi wa Taasisi hiyo.

Neema alisema mafunzo hayo yalikuwa ya wiki moja ya utengezaji sabuni, Mafuta ya kupaka, na sabuni za maji ambapo kila mshiriki amepewa Cheri cha ushiriki kwa kufanya vizuri ambapo kwa sasa anamiliki Kiwanda chake.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: