Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof Adolf Mkenda akifungua kikao cha tathimini ya maonesho ya utalii ya karibu kusini jana kilichojumuisha makatibu tawala wa mikoa yote ya nyanda za juu kusini leo ,kulia kwake ni mwenyekiti wa makatibu tawala Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happines Seneda
Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Prof Adolf Mkenda akionyesha jarida la kuelezea vivutio vya utalii kusini
Mwenyekiti wa kamati ya Ma Ras ya utalii kusini ,Ras wa mkoa wa Iringa Happines Seneda akieleza faida ya maonesho ya utalii ya karibu kusini
mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini na msemaji wa wizara ya maliasili na utalii Dorine Makaya kulia kufuatilia kikao cha tathimini ya maonesho ya karibu kusini leo
Baadhi ya wadau wa utalii wakiwa katika kikao hicho
Kamishina mwandamizi wa hifadhi za Taifa (TANAPA) kanda ya nyanda za juu kusini Dkt Christopher Timbuka kushoto akifuatilia kikao cha tathimini ya maonesho ya utalii ya karibu kusini leo PICHA NA HABARI NA FRANCIS GODWIN
WIZARA ya maliasili na utalii imesema maonesho ya utalii ya karibu kusini yaliyofanyika mapema mwaka huu mkoani Iringa kwa ajili ya kufungua lango la utalii mikoa ya nyanda za juu kusini yameleta mafanikio makubwa kwa wawekezaji mbali mbali kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi kukusudia kuja nchini .
Akifungua kikao cha tathimini cha maonesho hayo leo katika ukumbi wa chuo kikuu cha Elimu Mkwawa kikao kilichoshirikisha makatibu tawala wa mikao yote ya nyanda za juu kusini na waalikwa kutoka mkoa wa Mwanza ,katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Prof Adolf Mkenda alisema kuwa kupitia maoneshi hayo wizara yake imejipanga kuona inazitumia changamoto zilizojitokeza kuona inaboresha zaidi maonesho kama hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika kanda ya ziwa .
" Tathimini hii inatupa fursa ya kujifunza changamoto mbali mbali na mafanikio yaliyotokana na maonesho yaliyopita na wakati mwingine tunapoandaa maonesho kama hayo basi kuweza kutumia changamoto hizo kuboresha zaidi ili kuweza kuvutia idadi kubwa ya wawekezaji na kuona Taifa linapata faida kubwa kutokana na sekta hii ya utalii nchini " alisema Prof Mkenda
Kuwa uongozi wa mkoa wa Iringa chini ya katibu tawala wa mkoa huo Happiness Seneda ambae alikuwa ni mwenyekiti wa maonesho ya karibu kusini waliweza kufanya kazi kubwa ya kuandaa maonesho hayo kwa kushirikiana na makatibu tawala wa mikoa yote ya nyanda za juu kusini na hata kuyafanya maonesho hayo kuliletea heshima kubwa Taifa hasa katika sekta ya utalii .
Alisema maonesho kama hayo yamekuwa yakifanyika hata mwaka juu yalifanyika kwa mikoa ya nyanda za juu kusini ila ubora wa maonesho ya safari hii umetokana na makatibu tawala wa mikoa ya nyanda za juu kusini kwenda Kujifunza kupitia maonesho ya utalii ya Kill Fair ambayo yamekuwa yakiendesha na sekta binafsi na kupitia ziara hiyo ya mafunzo kwenye maonesho hayo viongozi wa mikoa ya nyanda za juu kusini waliweza kutumia vizuri ziara na kuboresha maonesho ya karibu kusini .
Hivyo alisema kwa mwakani kwenye maonesho kama hayo wanategemea kuona mambo mazuri zaidi ya idadi ya wawekezaji inaongezeka zaidi kwani changamoto chache zilizojitokeza safari hii zitakuwa zimepunguzwa ama kumalizika kabisa .
Prof Mkenda alisema lengo la wizara yake ni kuona fedha za umma zinatumika vizuri na kuwa na mrejesho mzuri wenye kuliletea Taifa faida na sio kuliingizia Taifa hasara .
Alisema katibu tawala wa mkoa wa Iringa kama mwenyekiti wa maonesho ya karibu kusini na timu yake wameonyesha umakini mkubwa kwa kufanya maonesho mazuri kwa gharama nafuu na fedha zilizotengwa kwa ajili ya kazi hiyo kutumika na hata kubaki akiba jambo mbalo ni zuri sana hasa katika upande wa ubanaji matumizi katika uendeshaji wa shughuli mbali mbali .
" Niseme tu serikali inahitaji kuona matokeo makubwa yanakuwepo kwa gharama nafuu na kuepuka gharama na matumizi ya fedha yasiyo na ulazima katika kutangaza utalii nchini ndio maana kuna mtumishi wa mmoja wa bodi ya Utalii Nchini (TTB) niliweza kumsimamiasha kazi jumapili asubuhi baada ya kutaka kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni 70 kwa ajili ya kutangaza utalii kwa mtu ambae hakuna na mkataba wowote na wizara hatuwezi kutumia vibaya fedha kwani matumizi yasiyofaa katika wizara hayaisaidii wizara kupiga hatua na sisi tunataka kutumia fedha zenye mrejesho mzuri"
Katika hatua nyingine Prof Mkenda alisema kuwa kwa kuwa serikali imeamua kuendeleza utalii nchini wizara yake imejipanga kuendeleza utalii kwa kufungua milango ya utalii katika kanda zote za Tanzania tofauti na ilivyokuwa awali ambapo nguvu kubwa ilielekezwa hifadhi za kaskazini pekee .
Aidha alisema kupitia ukusanyaji wa mapato yatokanayo na sekta ya utalii kwa mara ya kwanza wameweza kutoa gawio la zaidi ya bilioni 4 serikalini jambo mbalo ni la kujipongeza na bado wameendelea kujipanga kuendelea kutoa gawio kubwa zaidi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa makatibu tawala wa mikoa ya nyanda za juu kusini Happines Seneda alisema kuwa pamoja na maonesho hayo kufana mwaka huu wamejipanga kuboresha zaidi mwakani na kuwa changamoto kubwa zilizokuwepo hasa juu ya Hoteli za wageni mkoa wa Iringa umeanza kutatua changamoto hiyo kwa kugawa maeneo ya ujenzi wa Hoteli zaidi za kitalii na baadhi wameanza kujenga hoteli za kisasa ambazo awali hazikuwepo .
Kamishina mwandamizi wa hifadhi za Taifa (TANAPA) kanada ya kusini Dkt Christopher Timbuka alisema kuwa kupitia maonesha ya karibu kusini mwaka huu idadi ya watalii na wawekezaji katika hifadhi za mikoa ya kusini ikiwemo ya Ruaha imezidi kuongezeka na wapo walioomba kuwekeza katika ujenzi wa Hoteli .
Post A Comment: