Thursday, 19 December 2019

WATAKIWA KUELIMISHA WATANZANIA NAMNA YA KUJIEPUSHA NA MAFURIKONa.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Wito imetolewa kwa wataalam wa Majanga ya asili hapa nchini  kutumia elimu yao vizuri kwa kuwafikia watanzania  ili kujiepusha na  majanga ya mafuriko na ukame  na si  kukaa na elimu ya kwenye makaratasi tu huku wananchi wakiumia.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma na Katibu mkuu ,Ofisi ya waziri mkuu ,anayeshughulikia Sera,Uratibu,Menejimenti  idara ya Maafa  Bi.Dorothy Mwaluko wakati akifungua warsha ya siku tatu ya mafunzo kuhusu upunguzaji wa madhara ya janga la  Mafuriko na ukame ijulikanayo kama “National Workshop On Risk Profile for Floods and Droughts  chini ya uratibu wa UNDRR.

Bi.Mwaluko amesema  haiwezekani wataalam wa majanga ya asili wanakaa kwenye vikao vya mikakati ya kuzuia majanga huku walengwa wenyewe hususan wananchi wa Kawaida wakiwa waathirika wa kwanza bila hata kufikiwa elimu husika.

“Haya mnayojadili yanaishia kwenye vitabu tu hayawafikii walengwa hivyo haiwezekani mnakaa tu kwenye vikao lakini hayo mnayojadili hayafiki popote lazima ifike mahali tuwe watekelezaji na si wasemaji tu huku wananchi wakiangamia ,sawa,Msipige Makofi mtapiga makofi kama mtafikia lengo la kuwasaidia wananchi mnakaa kwenye viti vizuri huku wananchi wanaangamia na mafuriko na ukame.

Mwaka mpya ukifika nataka nipate profile inayoelezea nini kifanyike katika kukabiliana na majanga na kitu gani kinakuja baadae,information is Power lazima niwanange na si kila siku kuwasifia”amesema.

Aidha ,Bi.Mwaluko amesema ni muda sasa umefika kwa wataalam wa hali ya hewa na  wataalam wa majanga ya asili hapa nchini  kuelimisha wananchi kujikita katika kilimo kwenye maeneo ambako mvua zinanyesha na si kwa kuvaa suti tu kila wakati hasa wakati huu wa masika huku pia akielekeza namna nzuri ya kutoa elimu ya kujikinga na mafuriko.

“Sasa hivi mvua zinanyesha  ,unaweza ukapita mtu hana hata jembe na wataalm mpo mnafanya nini?sasa hivi ukisikia mafuriko,mifugo wamekufa.amesema.

Kwa upande wao baadhi ya Washiriki wa warsha hiyo wamesema mabadiliko ya hali ya hewa yana athari kubwa kwa binadamu na viumbe hai wengine huku wengine wakishauri pia kuwa na mpango madhubuti wa kukinga maji ya mvua ili yasiwe yanapotea bure pindi mvua inaponyesha.
No comments:

Post a comment