Friday, 13 December 2019

Usalama Sc Kesho Uso kwa Uso na Wajukuu wa Chief Milambo.


Na John Walter-Babati

Kikosi cha Usalama Sports Club kutoka Mkoa wa Manyara kinashuka dimbani kesho saa kumi kamili jioni itaendelea na mchezo wa ligi daraja la pili kumenyana na Milambo Fc ya Tabora.

Mchezo huo utandazwa katika uwanja wenye nyasi za asili katika shule ya Sekondari Singe pembezoni kidogo mwa Mji wa Babati ambapo kiingilio kimetajwa ni shilingi elfu moja(1000).

Wakati wakishuka dimbani jumamosi hii Desemba 14, Usalama Sc iko nafasi ya 2 kundi B ya ligi daraja la  pili Tanzania Bara (SDL) kwa alama 7 baada ya kucheza mechi 4.

Timu hiyo imeshinda michezo 2,imepoteza mechi 1 na kutoa sare mchezo 1.

Usalama FC imefunga magoli 6 na kufungwa mabao 4 huku vinara wa kundi B wakiwa ni Kitayosce FC kutoka Tabora yenye alama 12 baada ya kucheza mechi 4.

Mechi zingine kesho kundi B ya SDL,Bulyanhulu ya Shinyanga watawaalika Kasulu Redstar katika uwanja wa Taifa Mjini Kahama wakati Wanakisha mapanda Toto African watakuwa wenyeji wa Kitayosce FC katika uwanja wa Nyamagana Mwanza.

No comments:

Post a comment