Mwenyekiti wa Umojawa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Arusha Saipulani Ramsey amewataka vijana kujenga utamaduni wa kushiriki katika michezo kama njia ya kujenga umoja na mshikamano katika jamii na pia kuimarisha afya kupitia michezo.

Akizungumza katika bonanza la michezo la miaka 58 tangu Tanzania ipate Uhuru lililoandaliwa na Afisa Tarafa wa Elerai Titho Cholobi na kufanyika katika viwanja vya FFU kwa Morombo ,Mwenyekiti huyo amesema kuwa michezo hiyo imehusisha makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa serikali ,viongozi wa Ccm kuanzia ngazi ya mitaa na kata pamoja na Kundi la madereva ambalo ni kundi muhimu kijamii na kisiasa.

Amempongeza Afisa Tarafa wa Elerai kwa kuwa mbunifu na kuandaa michezo hiyo ambayo imekua kiunganishi kikubwa kati ya chama na wananchi,pamoja na serikali na wananchi na kuwataka viongozi wengine waige mfano wake.

Afisa Tarafa ya Elerai Titho Cholobi amesema kuwa michezo mbalimbali imefanyika ikiwemo mpira wa miguu ,kuvuta kamba,kukimbia na mayai pamoja na mbio za magunia lengo ikiwa ni kuwaleta wananchi pamoja na kimarisha mahusiano bora kati ya viongozi wa serikali na wananchi pamoja na viongozi wa chama na wananchi.

Cholobi anasema kuwa michezo hiyo itaandaliwa Mara kwa Mara pia inasaidia kukuza vipaji na kuwaepusha vijana na makundi ya mabaya ya uhalifu kwa kujikita katika michezo na mazoezi kwa ujumla.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Muriet,Paulo Sanka  ambaye ni mmoja kati ya waandaji wa Bonanza hilo amesema kuwa amefurahi kuwa karibu na wananchi  ili kuweza kushirikiana katika utatuzi wa kero na kuleta maendeleo kwa pamoja.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: