Mbunge wa Segerea Mhe Bonah Ladslaus akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mivinjeni Kata ya Buguruni kikao kilichokuwa kikijadili usalama 
Mwenyeki wa Serikali za mtaa Mivinjeni Kata ya Buguruni Fadiga Legele akizungumza katika kikao cha Serikali za Mitaa kujadili maswala ya Ulinzi na Usalama 


MBUNGE wa Segerea (CCM )  Bonnah Ladislaus ameshangazwa  na wimbi la raia wa kigeni wanaosadikika kuishi mtaa wa Mivinjeni  Kata ya Buguruni Halmashauri ya Ilala  na kushaur Idara ya Uhamiaji wafanye uchunguzi wa kina katika eneo hilo kuangalia kama wana vibari vya kuishi nchini au la.Mwandishi Heri Shaaban anaripoti 


Mbunge Bonah alipatwa na hofu hiyo  jana katika ziara yake kata ya Buguruni Mtaa wa Mivinjeni kwenye mkutano ulioandaliwa na mwenyekiti  wa Serikali ya Mtaa wa Mivinjeni  Fadiga Legele.

Alipongeza Serikali ya Mtaa wa Mivinjeni kumwalika  katika mkutamo huu wa  wananchi ambapo walikuwa  wakijadili maswala mbalimbali likiwemo la ulinzi na usalama.

"Kiukweli nimeshtushwa na taarifa ya raia wa kigeni zaidi ya 300 kuishi mtaa huu, kuna umuhimu wa idara ya Uhamiaji kufanya oparesheni kabambe   katika Kata hii kwa ajili ya usalama wa wananchi wangu na wapiga kura wangu  tukielekea katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwishoni mwa mwaka ujao 2020. lazima kuhakikisha usalama unakuwepo ndani ya Jimbo langu la Segerea alisema Bonah.


Alisema jimbo hilo la Segerea lina wakazi milioni 1.4 Mitaa 61  hivyo wananchi washirikiane na wenyeviti wa Serikali za mita katika utoaji wa taarifa za kero ili zifike kwa wakati  na kutatuliwa na Serikali.

"Katika  juhudi za kumsaidia Rais wetu John Magufuli kujenga Tanzania ya viwanda naomba wananchi wenzangu jimbo la segerea tushirikiane kwa pamoja tuweze kujikwamua kiuchumi." alisema. Bonnah.

  Awali mwenyekiti mpya wa Mtaa huo Fadiga Legele akisoma taarifa ya Mtaa alisema mtaa wake una wakazi 17,000 kwa sasa ambao ni watanzania na raia wa kigeni kwasasa tishio lililokuwepo kuna wimbi la Raia  wa kigeni zaidi ya 300 ambapo hulala chumba kimoja watu 20 hadi 30 .

Fadiga alisema mara baada kuingia madarakani ajenda yake ya kwanza ilikuwa ni kuimalisha ulinzi wa mtaa ili eneo hilo wananchi wake waishi kwa usalama  na Mali zao .

" Leo ni kikao cha ulinzi na usalama, pamoja na mambo mengine tutahadili  katika kikao hiki kuhusu maelekezo ya serikali kwa wamiliki wa nyumba zote. Serikali inawaagiza wenye nyumba kupangisha nyumba zao kwa kutumia miongozo iliyo katika mikataba maaulum itakayopatikana kwenye ofisi za Serikali za mitaa, mikataba hiyo itatolewa kwa wamiliki wote wa nyumba Mtaa wa   Mivinjeni bure" alisema Fadiga.

Kwa upande wake mtendaji wa mtaa wa Mivinjeni  Uwesu Bakari  alisema madalali wote wa nyumba eneo hilo lazima wajisajili Ofisi ya mtaa na dalali atakaye kiuka agizo hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha uwezo alisema pia kutokana na taratibu Ilizowekwa na serikali kuanzia sasa itakuwa ni marufuku kwa wamiliki wa nyumba kupokea wapangaji bila kitamburisho cha uraia, cha mpiga  kura au Leseni mpangaji aliyekosa viambatanisho hivyo marufuku kumpangisha.


Kikao hicho pia kimepitisha ada ya ulinzi Shirikishi kila kaya 1000 baa na fremu za Biashara shilingi 5000.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa Uhamiaji Ilala Lukumay Emanuel alisema wamepokea taarifa ya Mbunge Bonah kuhusiana na raia wa kigeni wataifanyia kazi haraka na kuomba ushirikiano kwa wananchi.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: