Tuesday, 31 December 2019

Manyara yashika namba moja Kwa usafi


Na John Walter-Manyara

Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Manyara yanyakua Kikombe na Kitita cha shilingi Milioni Tatu baada kung’ara katika mashindano ya jumla ya Usafi na Mazingira na kuipiga chini Mikoa Mingine.

Akikabidhi zawadi hizo kutoka ofisi ya wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Missaile Mussa amesema mashindano hayo yalihusisha Mikoa Mitatu Ya Manyara,Arusha na Katavi.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema mkoa huo hausifiki kwa usafi tu bali katika Usalama na kila idara wapo vizuri.

 Ameongeza kuwa 'sisi sio watu wa maneno tunapiga kazi,ingekuwa ni mikoa mingine wangezungumzia Ushindi huu mwaka mzima' alisema Mnyeti.

Naye  Katibu wa Afya mkoa wa Manyara Thomas Malle  anasema mafanikio hayo wameyapata kwa sababu wanazingatia kanuni zote za Usafi ambazo zinafanywa na kampuni walizozipa kazi.

No comments:

Post a comment