Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, ameagiza kukamatwa kwa Kapteni Mstaafu mkoani Kilimanjaro John Mushi, kwa madai ya kumiliki kwa mabavu eneo la TANESCO kwa zaidi ya miaka 35, huku akiwa halipii kodi ya ardhi anayodaiwa ambayo ni zaidi ya Milioni 20.

Eneo hio lenye ukubwa wa mita za mraba 3,371 mali ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linadaiwa kumilikiwa na Mushi tangu mwaka 1984 huku kodi ikilipwa na Tanesco. Anadaiwa hana nyaraka zozote zinazomruhusu kufanya hivyo.

Sabaya pia ameagiza mali zilizokuwepo katika eneo hilo vikiwamo vifaa vya ujenzi kuzuiwa na mashine ya kufyatua matofali kupelekwa katika eneo la ofisi yake mpaka  Mushi atakapolipa kodi ya miaka 35 aliyolipiwa na Tanesco

Sabaya ametoa agizo hilo jana Jumatatu Desemba 2, 2019 baada ya kutembelea eneo hilo, kutoa siku 30 kwa Tanesco kuhakikisha wanazungusha ukuta eneo lote na siku 60 kuanza ujenzi wa jengo la kisasa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: