Tuesday, 31 December 2019

DC MTATIRO ATOA AGIZO KWA MAOFISA UGANI TUNDURU


Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro akizungumza leo katika kikao 
MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Julius Mtatiro amewataka maafisa Ugani wa Wilaya hiyo katika msimu wa mwaka 2020 kuweka mpango kazi ambao unaoonyesha utendaji kazi wao dhidi ya Wakulima ili wakulima hao wazalishe  mazao yao kwa tija .mwandishi Amon Mtega anaripoti kutoka Tunduru

Wito huo ameutoa wakati akifungua mdahalo ambao uliandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na msaada wa Kisheria  katika kituo cha Tunduru  mkoani humo (TUPACE) ambao ulihudhuliwa na watalaamu mbalimbali wakiwemo wa Sekta ya Kilimo wa Wilayani humo.

 Mtatiro akizungumza wakati wa ufunguzi huo amesema kuwa wakulima waliyowengi wamekuwa wakipata hasara kwenye mazao yao pindi wanapozalisha mashambani ni kutokana na wakulima kukosa msaada wa elimu kutoka kwa watalaamu wa Kilimo (Maafisa Ugani) jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma kimaendeleo.

  Kufuatia hali hiyo Mtatiro amesema katika msimu wa kuanza mwaka mpya kila Afisa Ugani aweke mpango kazi ambao unaonyesha kuwa amewahudumia wakulima wangapi katika kipindi cha mwaka mzima unaoanza sasa pamoja na kuweka namba za simu za wakulima hao ili mwisho wa siku kubaini kama wakulima wamepata tija au laa.

 "Mimi nawambieni ukweli siwezi kuona wakulima wanahangaika namna ya kupata huduma za watalaamu wa Kilimo huku ninyi mpo  mmejifungia maofisini tuu nasema sikubali kabisa na mtaniona mbaya" amesema mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Asasi hiyo ya TUPACE ,John Nginga awali amesema kuwa lengo la mdahalo huo ni kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wakifuatilia utekelezaji wa miradi ya Kilimo has a cha umwagiliaji pamoja na ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za Umma .

 Nginga amesema kuwa mradi huo wa ufuatiliaji wa rasilimali za Umma katika sekta ya Kilimo umefadhila na shirika la Foundation For Civil Society (FCS)ambapo wamebaini licha yakuwepo kwa utekelezaji ila changamoto wakulima wengi hawana elimu ya Kilimo jambo ambalo linawafanya walime kwa kutumia uzoefu.

 Naye kaimu Afisa Kilimo Wilaya ya Tunduru Methodi Pilli alisema kuwa changamoto iliopo kuwa sikimu za umwagiliaji hadi sasa zipo tano(5)ambazo nazo wakulima wake wamekuwa hawazitumii ipasavyo hasa katika Kilimo wanalima mara moja badala ya kulima mara mbili kwa mwaka.

 Aidha Pilli amesema kuwa wamejipanga kikamilifu katika suala la utoaji Elimu kwa wakulima licha ya idara kukabiliwa na uchache wa watumishi ambao baadhi yao wamekuwa wakishindwa kuwafikia wakulima mashambani kwa wakati.

Hata hivyo aliwataka wakulima kuacha kununua dawa za kutibu mimea kwa mazoea na badala yake kabla ya kununua waweze kupata maelekezo sahihi ya dawa hizo ili kuepusha kuyaathili mazao.

No comments:

Post a comment