Wafanyakazi wa Kampuni ya tecno road wakiwa pamoja na balozi wao mpya casto Dickson wakati wa kutambulisha huduma mpya ya usafiri kutoka Mkoa mmoja hadi mwengine.

 
KAMPUNI ya Tecno road watambulisha huduma mpya ya usafiri kwa abiria wa mikoani.

Akizungumza na waandishi wahabari Muwakilishi kutoka Kampuni hiyo Rashid Balewa amesema huduma hiyo mpya ya usafiri kwa abiria wa mikoa hadi Mkoa (get a ride) itawasaidia abiria kuchangia gharama ndogo kwa dereva mwenyewe gari binafsi nakumuwezesha kufika mkoa anaosafiri kwa bei nafuu na usalama zaidi.

"Kupitia huduma hiyo abiria anaweza kupakua mtandao na kujisajiri kupitia namba ya simu na kumuwezesha kupata usafiri haraka zaidi na salama kutokana na kuwepo kwa taarifa ya gari binafsi iliyopo karibu yake,"

Kwa upande wake Balozi wa huduma hiyo (get a ride) Castro Dickson amefafanua sababu za yeye kupewa shavu la ubalozi na kuaminiwa kutangaza huduma hiyo.

"Shughuli zangu za kila siku zinanipelekea kutumia usafiri na hasa katika kipindi changu cha siz kitaa nakutana na watu mbalimbali na tofauti tofauti hivyo najua vitu gani wananchi wanavihitaji ili kuwarahisishia maisha kwani hakuna sehemu utahitaji kwenda bila usafiri wa haraka na nafuu hasa ukizingatia Safari za mikoani,"

Pia Dickson amewapa ushauri wasanii, watangazaji kufanya kazi kwa bidii hasa wanapopewa ubalozi wa bidhaa yoyote ile kwani Kampuni inaona mbali na kumchagua asimamie bidhaa hiyo ili kuitengeneza Kampuni uaminifu kwa jamii na hata kuongeza kipato katika Kampuni kwa wepesi.

"Kuna baadhi ya watu huchukulia ubalozi Kama sehemu ya kupiga pesa hivyo tujaribu kujitengenezea unidhamu wa kazi ili tuendelee kuheshimika kwenye makampuni mengine,"


Wafanyakazi wa Kampuni ya tecno road wakiwa pamoja na balozi wao mpya casto Dickson wakati wa kutambulisha huduma mpya ya usafiri kutoka Mkoa mmoja hadi mwengine.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: