Monday, 16 December 2019

Bunge SC yafufua matumaini ya Ubingwa Huku Burundi wakiona cha moto kwa Bunge Queens, yabugizwa 78-15


Wakichagizwa na Uwepo wa Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ambaye alilazimika kuingia chumba cha kubadilshia nguo (changing room)  kuwaongezea hamasa wachezaji, Bunge SC maarufu kama Ndugai Boys imewalaza Bunge la Kenya kwa bao 1-0 katika mchezo mkari na uliojaa ufundi mwingi.

Ushindi umetokana na bao lililofungwa na Ally King (Jang'ombe)  kufuatia krosi iliyopigwa na Alex Gashaza (Ngara)  ambaye awali alipenyezewa mpira na Venance Mwamoto (Kilolo).

Kwa ushindi huo Bunge la Tanzania imefikisha point sita na imefufua matumaini ya kutwaa ubingwa au kumaliza nafasi ya Pili kwani tayari Uganda watakayokutana nayo jumatano ina point tisa.

Awali katika netball Bunge Queens iliweka rekodi ya kufunga magoli mengi baada ya kuichakaza Burundi kwa magoli 78-15.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge SC William Mganga Ngereja, matumaini ni makubwa kwa Tanzania kuibuka mshindi wa jumla hasa baada ya jana kuzoa medali zaidi ya tano za dhahabu kwenye riadha na kushika nafasi ya Pili kwenye mchezo wa kuvuta Kamba

No comments:

Post a comment