Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli amewataka watanzania kuepuka kuwasikiliza vibaraka wa ndani ya nchi wanaotumiwa na Mabeberu kutoka Mataifa ya nje kuharibu sifa njema ya
Taifa la Tanzania.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Nov.21,2019 katika mahafali ya chuo kikuu cha Dodoma yaliyokwenda sambamba na zoezi la Kutunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari Falsafa ambapo amesema kwenye Mafanikio na Changamoto zipo ,hivyo amebainisha hatokatishwa tamaa na Mabeberu huku akiwataka watanzania kuwa na mshikamano na Uzalendo kwa Maendeleo Taifa .
Rais Dokt.Magufuli amesema Tanzania ina vivutio vingi ambapo duniani kote Nchi ya Tanzania ni ya Pili kwa vivutio vya utalii na ni nchi ya pekee Duniani yenye Madini ya Tanzanite hivyo amewataka watanzania Kuacha kulalamika kwani Tanzania ni tajiri na kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii.
Aidha,Rais Dokta.Magufuli amesema Uchumi wa Tanzania Unaendelea kuimarika ukikua kwa asilimia saba[7}na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano zinazokua kiuchumi kwa kasi miongoni mwa nchi
Tano{5]barani Afrika.
Rais Magufuli ni wa tatu kutunukiwa Shahada ya heshima ya Udaktari wa Falsafa [ Honorary PhD] , ambapo wa kwanza ni aliyekuwa Waziri Mkuu miaka ya 1962 hadi 1977 Hayati Rashid Mfaume Kawawa akifuatiwa na
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete .
Post A Comment: