Na Avitus Benedicto Kyaruzi,Kagera.
Zaidi ya shilingi milioni 74 zimetolewa na mbuunge wa jimbo la Muleba Kaskazini mh Charse Mwijage katika kuchangia maendeleo ya kata Kamachumu  iliyopo Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
 
Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo hilo Mh Charse Mwijage Nov 20, 2019 wakati akiongea na wananchi kwenye ufunguzi wa kuwatambulisha na kuwanadi wagombea wanao wania nafasi mbalimbali katika  uongozi wa serikali za mitaa kupitia chama cha mapinduzi CCM Wilayani humo mkutao uliofanyika katika kata ya  Kamachumu.
 
Aidha Mh Mwijage amesema kuwa licha ya yeye kuchangia kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kuunga mkono jitihada za kuchangia maendeleo kwenye kata hiyo ameongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh John Pombe Magufuri kwenye kata hiyo.
 
Mbali na kiasi icho pia mh Mwijage amechangia ujenzi wa vyumba vinne pamoja na mabati 180,katika hospitali ya Ndorage iliyopo Wilayani humo.
 
Ameongeza kuwa wananchi wa jimbo hilo watazidi kunufaika na miradi mbalimbali ya kimaendeleo uku akitaja uzinduzi wa Chuo  Cha Ufundi  Cha Wilaya Ya Muleba Veta kitakacho funguliwa  rasmi na Waziri wa Elimu Mh Joyce Ndalichako mnamo tarehe 28/11/2019.
 
Amewataka viongozi watakao chaguliwa  kupitia chama hicho kufanya kazi kwa bidii na kufuata sheria na ilani ya chama cha Mapinduzi ili kuwaletea wananchi maendeleo pasipo kufuata kabila wala itikadi za kisiasa.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Kata ya Kamachumu bwana Abdunuru Bengesi amesema kuwa ana mashaka na viongozi wanao wania nafasi hizo kwa kuwa walio wengi wana uzoefu katika uongozi na kuongeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa viongozi hao watapewa semina elekezi ili kuweza kufanya kazi kuendana na kasi ya mh Rais.
 
Kwa upande wa wananchi wa kata hiyo wamempongeza mbunge wao kwa juhudi kubwa anazo zifanya za kuwaletea maendeleo huku wakihaidi kumpatia ushirikiano katika Chuo  Cha Ufundi  Cha Wilaya Ya Muleba Veta kwa kuwapeleka watoto wao kupata ujuzi mbali mbali katika chuo hicho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: