Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akizungumza na mabalozi wa Kata ya Minyughe wilayani Ikungi mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi hao.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu ameendelea na ziara ya kukutana na wajumbe wa nyumba kumi (Mabalozi) katika jimbo hilo kwa ajili ya kuzungumza nao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Katika ziara hiyo Kingu amekuwa akikutana na mabalozi, wazee na wajumbe wa jumuia zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kufanya nao mazungumzo ya kuimarisha chama hicho na kusikiliza changamoto zilizopo na kuzijadili na kuzitafutia ufumbuzi.
Akizungunza na mabalozi wa Kata ya Minyughe aliwataka kudumisha mshikamano na kuondoa tofauti zao kama zipo ili kukipa ushindi mnono chama hicho katika uchaguzi huo.
" Sina wasiwasi kwa hapa Minyughe najua mpo vizuri hamna migogoro kama ilivyo katika maeneo mengine ninawaamini na viongozi wenu wamejipanga kukupigania chama chetu" alisema Kingu.
Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Issa Mussa Mkuki alitoa onyo kwa wanachama wa chama hicho ambao watabainika kukisaliti katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi.
" Mwanachama wetu yeyote atakaye tusaliti hatuta mvumilia tutamchukulia hatua za kinidhamu" alisema Mkuki.
Kingu ameendelea kufanya ziara katika jimbo hilo ambapo jana alikutana na wazee pamoja na vijana wa Kata ya Puma na kuzungumza nao.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: