Friday, 1 November 2019

Kijana Aliyemtishia Mwenzake Kwa Bastola Yamkuta Mazito....IGP Amtaka Ajisalimishe Polisi

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amemtaka kijana aliyemtishia mwenzake bastola kuripoti polisi baada ya kuonekana akifanya kitendo hicho katika picha za video zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Mbali na kuripoti, Sirro amesema anatakiwa kusalimisha silaha yake.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu inayolenga kukomesha rushwa barabarani.

Sirro amesema ameagiza kukamatwa kwa kijana huyo lakini amekuwa akipiga chenga,  amemtaka akajisalimishe mwenyewe kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani.

IGP Sirro azungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya kupambana na rushwa barabarani.

See Police Force TZ's other Tweets

No comments:

Post a comment