Saturday, 30 November 2019

JUMUIYA YA WAZAZI WATAKA WAGOMBEA UBUNGE WACHAGULIWE NA JUMUIYA YAO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Edmund Mndolwa akimpa zawadi Makamu Mwenyekiti wa CCM  Bara Philip Mangula katika kongamano la chama hicho 
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi pamoja na chama cha Mapinduzi wakiwa katika Kongamano la Jumuiya
Mjumbe wa kamati ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Abdalah Othiman (kushoto)akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Ilala Baraka Obama katika kongamano la wazazi .

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Taifa Khery James akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kivukoni Sharik Choughule katika Kongamano la jumuiya Wazazi Taifa 


PICHA NA HABARI HERI SHAABAN

JUMUIYA ya wazazi  Chama cha Mapinduzi (CCM  ) Taifa wametuma maombi kwa Mwenyekiti wa ccm  Taifa Rais  John Magufuli wakitaka Wabunge wa kundi la Jumuiya ya Wazazi pamoja na madiwani wachaguliwe na Baraza Kuu la Jumuiya  hiyo.

 Mapendekezo hayo  ya ushauri kwa Rais John Magufuli yalisomwa katika hotuba na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa  Dkt,Edmund Mndolwa  wakati wa Kongamano la kumpongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa Mwenyekiti wa SADC na utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mndolwa alisema kwa sasa Wabunge wa kundi la wazazi wawakilishi Bungeni wanachaguliwa na baraza kuu la Umoja wa Wanawake UWT   wakati jumuiya ya wazazi inawajua watu wake vizuri  katika kukisaidia chama.

'"Desemba 2017  ulipokuwa ukifungua Mkutano Mkuu wa Wazazi Taifa uliofanyika Dodoma ulituahidi ombi letu la kuongezewa Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum wanaotokana na jumuiya yetu ulilipokea ukasema unagawanya viti   hivyo kwa jumuiya zote tatu  hivyo tunakumbusha agizo letu"alisema Mndolwa.

Mndolwa alisema  mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi  Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani  hivyo kama jumuiya wameomba watangaziwe mapema kuwajulisha wanachama wa jumuiya ya wazazi   wabunge wawili bila madiwani pengo kubwa sana.

Aidha alisema jumuiya ya wazazi ndio inajua wawakilishi wanaofaa kama watachaguliwa na jumuiya nyingine sio vizuri.

Wameshauri wagombea wote wapitie katika mchakato wa chama chao mwisho waishie katika Baraza la Wazazi Taifa kwa niaba ya mkutano mkuu.

Wakati huohuo Mndolwa alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais John  Magufuli  kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC uteuzi huo unakwenda sambamba na uadilifu wako,uzalendo wako , uchapakazi na utendaji kazi wako mahili.

Pia Jumuiya ya Wazazi Taifa wamempongeza Rai s Magufuli kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM  ujenzi wa barabara za juu ,ujenzi wa daraja jipya mto wami  pamoja na miradi mkakati katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Philip Mangula amezitaka Kamati za siasa  za Chama cha Mapinduzi wawe na siri katika kupitisha majina ya wagombea wasiwe wanatoa siri za chama .

Mangula alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi mwakani amezitaka kamati za siasa kufuata sheria na kanuni wawe na kifua cha ujasiri wasitoe siri za wagombea waliopitishwa  na kamati ya siasa wakati wa kujadili majina.

"Chama chetu kinaelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2020  naziomba kamati za siasa zote kuacha ushabiki wa  kukumbatia wagombea wakati wa mbio za kampeni bado"alisema Mangula


No comments:

Post a comment