NA HERI SHAABAN.

DIWANI wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo amewataka Wazazi kusomesha watoto wao katika shule za awali kwa ajili ya kuwajengea msingi mzuri watoto kabla kuanza darasa la kwanza.

Diwani Neema aliyasema hayo wakati wa mahafali ya shule ya awali ya Avemaria ambapo jumla ya wanafunzi 50 wa darasa la awali walikabidhiwa vyeti kwa ajili ya kuhitimu elimu hiyo.

"Wazazi wangu wa manispaa ya Ilala mtoto anapotimiza umri wa miaka mitatu nawashauri wapelekwe katika shule za awali anaposoma katika shule hizo unamjengea msingi  mzuri wa kujiamini pindi anapoanza darasa la kwanza anakuwa na uelewa"  alisema Neema .

Aidha alisema siri ya ufaulu kwa Wanafunzi wa darasa la saba  kushika nafasi za juu Kitaifa katika matokeo ya elimu msingi Halmashauri ya Ilala inatokana na Wazazi kuwandaa watoto wao kuanzia elimu ya awali na ushirikiano wa walimu katika kuzingatia masomo  sekta ya elimu msingi.

Alisema   ushirikiano wa wazazi , Walimu sekta ya  elimu msingi imekuwa kwa kasi katika wilaya ya Ilala ,ambapo ameeataka wazazi kujenga tabia ya kukagua daftari za wanafunzi wanapotoka shule.

   Alimpongeza Rais John Magufuli kuleta elimu bure katika serikali ya awamu ya tano kuanzia elimu ya Msingi hadi sekondari kwa sasa wanafunzi wanasoma  na wazazi wao wanawandeleza  kiwango cha elimu kimekuwa na shule za kata za Serikali zinafanya vizuri kwa sasa.

Amewataka wazazi wa Manispaa ya Ilala kupeleka watoto wao katika shule ya awali  Avemaria ili kwa ajili ya kuwaandaa wanafunzi kabla kuanza darasa la kwanza .


Kwa upande wake Donard Embele mmoja wa mzazi aliyesoma mtoto wake  Avemaria ameishauri Serikali kutoa ruzuku kwa shule binfsi za elimu ya awali kwa ajili ya kusaidia kujiendesha ili wapunguze viwango vya ada wazazi wamudu gharama za kusomesha.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: