Thursday, 28 November 2019

DC ASIA ABDALLAH:NILIPOKEA VITISHO NIKIPIGANIA HAKI ZA WANYONGEMkuu wa  wilaya ya  Kilolo mkoa wa  Iringa  Asia  Abdallha  (pichani)amesema amepata  vitisho vingi sana hata  kulimwa  barua  na mwanasheria  wa Halmashauri ya  Kilolo wakati akitekeleza majukumu yake ya  kupigania  wananchi wa  kijiji  cha Magome kupata ardhi yao zaidi ya hekari 300  walizokuwa  wameporwa na dalali wa  kijiji .

Akizungumza    jana kwenye  mkutano wa hadhara  kijiji  cha Magome   alisema kuwa  kazi yake kama mwakilishi wa Rais kwa ngazi ya  wilaya  ni  kuendelea  kuwatumikia  wananchi wa  Kilolo tena  bila  kutaka  malipo  yoyote  kwani mshahara  ambao analipwa  na serikali unamtosha kuwatumikia  wananchi hao 

Alisema sakata   hilo la ardhi  Zaidi ya hekari 300 ambazo mwananchi mmoja aliyefahamika kwa  jina la Kisoma alitaka kuwatapeli  wananchi  wa  kijiji  hicho na kuuza kwa makampuni ya kigeni  ya miti yaliyopo  wilaya ya  Kilolo ,lilipelekea kulimwa  barua na mwanasheria  wa Halmashauri ya  Kilolo akimtaka  kutoingilia kati  kuwatetea  wanyonge hao ila kesi  hiyo baada ya kwenda mahakamani ushindi  ulirudi kwa  wananchi  hao .

Kuwa  alipambana  kufa na  kupona na hata  kuhatarisha   maisha  yake kutoka kwa dalali   huyo  wakati akitekeleza  wajibu  wake wa  kupigania haki ya  wananchi iliyokuwa imeporwa na  dalali   huyo kwa maslahi yake binafsi .

Hivyo  alitaka  kuanzia  sasa    wawekezaji wanaofika Kilolo ni lazima  kufuata  taratibu za  uwekezaji kwa kupitia  kituo  cha  Taifa  cha  uwekezaji  ama ofisi ya mkoa na  wilaya    sio  kwenda  moja kwa moja  kijijini  kutaka  kuwatumia madalali  kuchukua ardhi ya  wananchi .

Mkuu  huyo wa wilaya  alisema  ofisi yake  imekuwa ikifanya kazi bega kwa bega na ofisi ya  mkoa wa Iringa  chini ya mkuu wa mkoa Alli Hapi na katibu tawala Happines Seneda kuona  wananchi wa  wilaya ya  Kilolo  wanafanya  shughuli  zao kwa amani na utulivu na kero  mbali mbali  zinapojitokeza  zinashughulikiwa  haraka
 
Kwa upande  wake mkazi wa kijiji cha Magome mzee   Amon Mtagi(84)  ambae alisaidiwa na  mkuu wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdallah kupata ardhi yake aliyoporwa na mtumishi   wa umma mstaafu  asema kama  ingekuwa  inawezekana Mungu aanze  kumchukua  yeye kwanza mkuu  huyo wa wilaya  abaki aendelee  kumsaidia  Rais Dkt  John Magufuli  kutetea  wanyonge .

“Mimi  na  wananchi  wenzangu wa kijiji  hiki  cha Magome  tuliumizwa  sana na uporaji  wa  ardhi  aliotaka kuufanya  msaafu  huyu  wa umma  ambae  alichukua sehemu  kubwa ya  ardhi ya kijiji  na  sisi  wanyonge  kukosa ardhi tulizunguka  sana kwa  viongozi mbali mbali  na  wakati  huo mkuu wa  mkoa wa  sasa Alli Hapi  alikuwa hajafika   ila  hatukusikilizwa ila  binafsi nakushukuru  sana mama Asia Abdallah  wewe  ulisimama mbele  kututetea na  tumepata  haki zetu “  alisema mzee  huyo  huku akitokwa na machozi ya   furaha

Kuwa amani ya  wananchi wa  kiiji  hicho ambayo  ilitaka  kutoweka kwa  wananchi  kutaka  kumvamia mstaafu  huyo kwa mapanga ilirejea  na Imani yao kwa serikali ya Rais Dkt  Magufuli   imezidi  kuongezeka  Zaidi  baada ya kutetewa  kupata  ardhi yao  waliyokuwa  wametapeliwa na mwananchi  huyo  mmoja .

“Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo wewe  umekuwa ni mkombozi  wetu na  mtetezi mkubwa wa wanyonge katika  wilaya  hii ya  Kilolo nakumbuka siku  ile  nilipokuja  kufuatilia ardhi yangu baada ya  kuzunguka  sana sikuwa  tena na uwezo wa kifedha hata  kurudi  nyumbani ila ulinisaidia mimi na wenzangu  kupata ardhi yetu hekari Zaidi ya 300 zilizoporwa  pia ulisaidia  fedha  za kijikimu na kuweza  kurudi nyumbani sina  cha  kukulipa kwa niaba ya  wenzangu ila nasema kwa kuwa  mimi  umri  wangu  umekwenda na natamani   sana kama  inawezekana hata  leo Mungu  aanze  kunichukua  mimi na  wewe  mkuu wa wilaya uendelee  kubaki kutetea  wananchi  wanyonge  kama anavyofanya  Rais wetu mpendwa Dkt  John Pombe Magufuli “  alisema mzee   Amon Matagi


No comments:

Post a comment