Saturday, 2 November 2019

Bendera za CCM, Chadema zashushwa mji wa Moshi


Bendera za vyama vya Chadema na CCM  katika jimbo la Moshi zilizokuwa zimewekwa katika barabara na mitaa mbalimbali zimeshushwa na mgambo na maofisa wa Halmashauri  leo Ijumaa Novemba Mosi, 2019.
Uamuzi huo umeonekana kuwashtua viongozi wa vyama hivyo viwili, huku Chadema kikikitupia lawama CCM kuwa ndio kilichosuka mpango huo, wakati CCM wakiwataka Chadema kuacha propaganda.
Shughuli ya kushusha bendera hizo  imefanywa na mgambo na maofisa wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

No comments:

Post a comment