Monday, 28 October 2019

ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA KUGOMBEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KUANZA KESHO 0KTOBA 29,2019


Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo ametangaza siku maalum ya Uchukuaji wa Fomu za Kuwania uongozi Serikali za Mitaa kuwa ni kuanzia Kesho Oktoba,29,2019

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba ,28,2019 Jijini Dodoma Mhe.Jafo amesema zoezi la uchukuaji wa fomu hizo  pamoja na kuzirudisha litadumu kwa muda wa siku saba kuanzia Oktoba 29,2019 hadi Novemba 4,2019.
Hivyo Waziri Jafo amesema muda huo ni Muafaka kwawagombea mbalimbali kuchukua fomu  na kurudisha ndani ya Muda husika kama ilivyopangwa.

Aidha,Waziri  Jafo amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wamikoa kote nchini kuhakikisha wanasimamia suala la ulinzi ,usalama na amani katika zoezi hilo.
Fomu hizo zitatolewa katika ofisi za wasimamizi  Wa Uchaguzi ambao ni watendaji wa mitaa na  vijiji.

Hata hivyo,Waziri Jafo amesema nafasi mbalimbali zimezibwa pale ambapo pako wazi   kwa watendaji wa Mitaa na wapo watumishi wa umma wamekaimu
nafasi hizo.

Ikumbukwe kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika
Novemba ,24,2019.

No comments:

Post a Comment