Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Ikungi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Wilaya ya Ikungi kwa kuwapungia mikono.

Wanafunzi wakimpungia mikono Waziri Mkuu.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa meza kuu na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Killimbah (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi.
 Wananchi wa Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akimkaribisha Waziri Mkuu na kutoa taarifa fupi ya maendeleo.
 Madiwani wa Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe akizungumza.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akizungumza.


Na Dotto Mwaibale, Singida.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Halmashuri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida  kwa matumizi mazuri ya fedha za miradi zinazotolewa na Serikali.

Majaliwa alitoa pongezi hizo wilayani Manyoni wakati akizungumza na watumishi wa umma katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Singida juzi.

" katika mkoa huu ni Halmashauri moja tu ya Ikungi ndiyo inayofanya vizuri kwa matumizi ya fedha za miradi zinazotolewa na serikali" alisema Majaliwa.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wilayani Ikungi Majaliwa alisema serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika majimbo yote ya uchaguzi mkoani humo.

Alisema katika wilaya hiyo serikali imetoa fedha katika miradi ya maji, afya, barabara, elimu na umeme ambapo tayari mkandarasi yupo akiendelea na usambazaji wa nguzo.

Alisema lengo la serikali ni kuonana kila nyumba hata ikiwa ya udongo na ipo juu ya mawe inapata umeme ifikapo 2020 kwa gharama ya sh.27,000 tu huku nguzo za umeme zikisogezwa hadi ilipo nyumba ya mwananchi.

Majaliwa alitumia mkutano huo kuwataka watumishi wa umma kuchapa kazi kwa bidii na kutoa onyo kwa madaktari kuacha kuuza dawa zinazopelekwa katika vituo vya afya na zahanati na kueleza atakayebainika atajuta kwani hawatamuonea huruma.

Akisisitiza kuhusu elimu alisema hivi sasa Serikali inatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi Sekondari  hivyo mtoto yeyote anayetakiwa kuwa shuleni akikutwa yupo mtaani akizurura  mzazi au mlezi wake atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine Majaliwa amewataka wakuu wa polisi wa wilaya na mikoa kuacha tabia ya kuwazuia wananchi wanaokuwa na mabango yenye kero mbalimbali anapokuwa kwenye ziara zake za kikazi.

Kutokana na mji wa Ikungi kuanza kukua kwa kasi Majaliwa aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuchangamkia fursa kwa kukopa fedha katika taasisi za fedha na kujenga mahoteli na nyumba za kulala wageni  ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kwenye mkutano huo mkuu wa wilaya hiyo Edward Mpogolo na wabunge wa Singida Magharibi,  Elibariki Kingu, Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe walitoa shukurani kwa Rais Dkt.John Magufuli kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali na kuahidi kuwa katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na vitongoji ushindi utakuwa kwa wagombea wote kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Share To:

msumbanews

Post A Comment: