Tuesday, 8 October 2019

WANARIADHA WALEJE NCHINI KUTOKA DOHA,NAHODHA WA KIKOSI ATEMA NYONGO KWA VIONGOZI.

Na Lucas Myovela_Arusha.

Timu ya Taifa ya riadha hapa nchi imelejea usiku wa Octoba 7,ikiwa imetokea Doha huko Qatar baada ya kushiriki katika michuano ya riadha ya dunia iliyokuwanikifanyika Doha Qatar.

Timu hiyo iliondoka hapa nchini Octoba 2 ,2019 ikiwa na jopo la watu wanne wanariadha watutu pamoja na kocha wa timu ndiyo waliweza kwenda kushiriki michuano ya dunia ya riadha ambapo michuano hiyo ilishirikisha wanariadha wa timu za mataifa mbali mbali.

Akiongeana na wanaandishi wa habari wakati wa kuwapokea wanariadha hao walipo wasili katika ardhi ya Jiji la Arusha kutokea Doha kisha Nairobi Nchini kenya Afisa utamaduni wa jiji la Arusha Benson Maneno ameeleza kuwa mpaka sasa timu hiyo inakila sababu ya kupongezwa kwa kila hali na mali kwa hatua waliyofikia.

Pia Benson Maneno ameleza kwamba licha ya changamoto mbali mbali walizokutana nazo wanariadha hao bado waliweza kuhimili hali ya hewa kutokana na joto kali walilo kutana nalo lakini bado wameiwakilisha nchi katika michuano ya dunia  na kuleta heshima kubwa baada ya nahidha wa timu hiyo kumaliza mzunguko wote.

"Nikiwa kama Afisa utamaduni jiji hili la Arusha niwapongeze wanariadha wote pamoja na kocha wenu aliyekuwa nanyi beba kwa bega hadi dakika ya mwisho ingawa hamjaja na midani lakini hii ni heshima kubwa kwa taifa letu la Tanzania na sisi kama viongozi tupo tayari kuunganisha nguvu,umoja na ustawi wetu katika uongozi na usimamizi ili kuondoa changamoto katika timu ya taifa ya riadha kwa pale mtakapo hitaji msaada wetu katika jiji la Arusha". alisema Benson maneno.

"Mkiwa kama wanariadha bora hapa nchini lakini bado hamchoki kuliwakilisha taifa kimataifa niwaombe msikate tamaa wala kuvunjika moyo kwa namna yeyote ile maana nyinyi bado ni mabingwa na katika mashindano kuna matokeo matatu na hata haya matokeo mliyotupatia bado siyo mabaya kikubwa tu nikujua wapi tulipo kwama ili msimu ujao tuweze kutatua na kuchukua ubingwa". aliendela kusema Benson Maneno.

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo ya riadha hapa nchini Bw Andrew Samson Panga,ameeleza kwamba licha ya joto kuwa kali hadi kufikia hatua ya wanariadha wengingine kufunga barafu katika miili yao ili kupunguza joto pia walipata changomoto ya wanariadha wawili wa timu ya Taifa waliweza kuumia katika michuano hiyo na kupelekea kubakiza mkimbiaji mmoja kati ya watatu waliyo kwenda Doha.

"Vijana wetu wamepambana vya kutosha lakini changamoto tuliyopana ni vijana wetu kuumia ambapo Stephano Uche aliumia goti na badae mwariadha wetu Agostino Sulle alipata shida ya nyonga kwahiyo hawakuweza kufika mwisho au kumaliza mashindano na Alphonce Simbu aliweza kupambana hadi mwisho kama mlivyo weza kuona katika vyomba vya habati vya kimataifa kiukweli haikuwa kazi ndogo wala kazi rahisi". alisema kocha Samson.

"Kiukweli tuliyo fika pale tumejionea hali halisi ya pale Doha na kipindi tunakuja tulikuwa tunajiuliza tunarudi ingawa hatuna midani na niwashukuru sana kwa mapokezi haya mliyotupatia maana mmekuja kutupokea mbali na mmetukalibisha vizuri mapokezi haya yanatia moyo sana maana tumeshindwa lakini bado watanzania wapo na sisi ni jambo jema sana kushikamana". aliendelea kusema kocha Samson.

Pia nahodha wa timu hiyo ya taifa ya riadha Alphonce Simbu, ameeleza kuwa mbali ya wao kushindwa lakini ameweza kushika nafasi ya kumi na sita na kuweza kushiriki mashindano ya Olimpiki (Olympic) huko Tokyo 2020 na kuwataka viongozi wa riadha taifa kuwa wamoja na kuacha majungu na mapishano katika kuendeleza michezo ya riadha hapa nchi maana kwasasa kumekuwa na sito fahamu kubwa kwa viongozi hao tofauti na mwanzo.

"Kwa upande wangu nimshukuru kocha wetu kwa kuto kukata tamaa na kuwa nasisi bado hata tulivyo shindwa bado hajavunjika moyo ametupa moyo sana na kutusaidia kimawazo lakini kwasasa kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana kwa viongozi wetu wa riadha taifa ninaomba warudishe umoja wao maana hili jambo linatuvunja moyo wanariadha".alisema nahodha wa timu  Alphonce.

"Toka mwaka 2016 katika michuano ya Olimpiki (Olympic) na niliweza kushika nafasi ya tano lakini pia niliongea jambo hili katika michuano ya Sokoine ingawa ukiwauliza hata leo bado hawata kubali kwamba hawana ushirikiano ile ofisi ya chama cha riadha taifa haipo vizuri kiukweli nimekuwa nikiwaomba viongozi kupatana ni sawa na baba na mama hawaelewani Je? unadhani watoto watakuwa katika hali ipi?,mimi niwaombe viongozi wangu wakae pamoja hawatashindwa kujua changamoto zao ni zipi na kuzitatua lasi hivyo tutaelekea mahali ambapo siyo pazuri katika chama cha riadha hapa nchini". aliendelea kusema Aphonce.

No comments:

Post a Comment