Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka akiwagawia wateja wa benki hiyo keki wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA, Usman Isiaka akizungumza na wateja wa benki tawi la Nyerere jijini Dar es Salaam, ikiwani ni maadhimisho ya wiki ya wateja duniani



Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

TAASISI za fedha nchini, zimeshauriwa kubadilika katika kuwahudumia wateaja wao na kuacha kutoa huduma kwa mazoea wakati wanapotoa huduma kwa wateja wao, ili kuendana na kasi pamoja na ushindani uliopo kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ili kuweza kufanya vizuri kwenye soko la ushindani.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA-Tanzania, wakati benki hiyo ilipoungana pamoja na wateja wake katika kusherehekea wiki ya wateja duniani iliyofanyika tawi la Nyerere.

“Nashauri taasisi zinazotoa huduma za kifedha lazima zibadilike na kuacha kutoa huduma kwa mazoea badala yake ziwe na ubunifu unaoendana na kipindi hiki cha ushindani wa soko la teknolojia kwani usipofanya hivyo ushindani ni mkubwa sana,” alisema Isiaka

Alisema UBA wanayo furaha kuungana na wateja wao kusherekea siku ya huduma kwa mteja duniani kwa kuwa wao ndio wanafanya benki hiyo kuwepo na kuendelea kutoa huduma stahiki na zenye ubora kwa wateja wao kwenye matawi yao yote nchini .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ledgewood Investiment, Raymond Mubayiwa, alisema kuwa katika kipindi hiki cha kusherekea wiki ya huduma kwa wateja wamejifunza mengi ikiwamo kupata fursa ya kukutana na watoa huduma wao na kuzungumza nao kwa kina kuhusu masuala mbalimbali jambo ambalo kwao limewapa faraja kubwa.


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: