Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tomorrow limefadhili tuzo za walimu jiji la Arusha ambazo zilizotelewa kwa kutambua na kuthamini mchango wa walimu wanaofaulisha wanafunzi vizuri kwa alama za juu katika shule za msingi na sekondari za jiji la Arusha.

TFFT imekua na utamaduni wa kutoa tuzo za walimu kila mwaka jijini Arusha ambapo mwaka huu imeamua kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo jiji la Arusha na shule binafsi katika kuhakikisha kuwa tuzo za walimu mwaka huu zinafanikiwa .

Meneja wa Programu ya Mafunzo kwa walimu katika shirika hilo Noah Kayanda amesema kuwa wamedhamini kipengele cha Tuzo ya Mwalimu Mahiri ikiwa ni moja kati ya njia ya kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla.

Noah amesema kuwa TFFT itaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi ili waweze kuboresha mbinu za ufundishaji na ubunifu na kukuza ubora wa elimu.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro  aliyefika kutoa tuzo za Walimu amewapongeza wadau mbalimbali wa;liojitokeza kufanikisha tuzo za walimu wakiwemo TFFT ,Shule ya Lucky Vicent pamoja na wadau wengine kwani tuzo hizo zinalenga kuwatia moyo walimu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: