Na Lucas Myovela_Arusha.

Kufuatia kimbinga kilichotokea tarehe 01 octoba jijini Arusha kinasadikika kusabibisha maafa makubwa ikiwemo kuzama kwa mitumbwi miwili ya kitalii katika ziwa Momela liliopo katika hifadhi ya Taifa ya Arusha ( ANAPA )  wiliyani Arumeru mkoani Arusha.

Katika tukio hilo la kuzama kwa mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba watalii kutoka nchini Ujerumani kunusulika kifo baada ya mitwimbwi hiyo kuzama pamoja na muongoza watalii kutoka kampuni ya kitalii ya Wayo Africa aliyejulikana kwa jina la Samwel Gildati Mhina anayefanya kazi na kampuni ya kitalii ya Wayo Africa kutoonekana mpaka sasa huku zoezi la kuendelea kumtafuta likiendelea katika ziwa hilo.

Akithibitisha tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Koka Mhita amesema kuwa toka jana majira ya saa 8:45 mchana kimbunga kikubwa kilitokea katika kitongoji cha Momela katika kata ya Ngalenanyuki wilayani Arumeru na kuzamisha mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba watalii wawili raia wa ujerumani waliyokuwa wakiendelea na utalii ndani ya ziwa Momela ndipo walipo kutwa na dhahama hiyo.

Kamanda amesema kuwa watu watatu kati ya wanne wameweza kuokolewa ambao ni watalii wawili na muongiza watalii mmoja waliyokuwa ndani ya mitwimbwi hiyo  huku akiwataja kwa majina watalii hao ni Dr Rosenberger pamoja na mumewe Dr Tuemper Bern John wote raia wa ujerumani waliyoweza kuokolewa baada ya jitihada zao za awali za kutaka kujiokoa kuzaa matunda pamoja na muongoza utalii mmoja aliyefamika kwa jina la Yona Mosha.

Na kuongeza kuwa mpaka sasa muongoza watalii mmoja Bw Samwel Mhina (29) bado hajapatikana pamoja na mtumbwi wake huku jitihada za ukoaji kutoka katika kikosi cha zima moto mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Arusha na wilaya ya arumeru zikiendelea na kazi hiyo ya kumtafuta ambapo mpaka hivi sasa bado hajapatikana.

Pia kamanda ameeleza kuwa mbali na kimbunga hicho kuzamisha mitumbwi miwili pia kimeweza kuleta maafa makubwa kwa wananchi kwa kuaribu nyumba za makazi,nyumba za ibada paomja na miundombinu hasa miundo mbinu ya umeme.

MADHARA YA KIMBUNGA KATIKA MIUNDOMBINU YA TANESCO.

Akitoa taarifa za kuharibiwa kwa miundombinu ya umeme katika jiji la Arusha Mhandisi mkuu wa shirika hilo mkoani hapa Ronesiano Shamba ameeleza kuwa miti mikubwa iliyoanguka baadabya kung'olewa na na upepo mkubwa huo kutoka umbali wa zaidi ya mita nane hadi kutupwa katika nyaza za umeme katika maeneo mbali mbali katika jiji la Arusha.

Akitaja maeneo yaliyokubwa na uharibifu huo mkubwa huo wa miundombinu ya umeme ni wilaya ya Monduli yote,kata ya olasiti,Sombetini,Iliboru,Sokoni one,Kimandolu,Moivo,Moshono,Kijenge kwa maeneo ya jiji la Arusha pamoja na halmashauri moja ya Monduli ambayo yenyewe iliathira yote na mpaka sasa jitihada za kurudisha umeme zikiendelea.

Pia katika halmashauri ya Arumeru ni katika maeneo ya Kata ya Kikwe,Patandi pamoja na Usa River,huku garama zote za miuondombinu iliyo haribika  zikielezwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 400 mpaka sasa huku bado tathimini nyingine zikiendelea kufanyika.

Mbali na kimbunga hicho kuleta madhara makubwa hayo bado shirika la umeme Tanesco Jiji la Arusha linaendelea na jitihada za kurudisha umeme kwa maeneo ambayo bado hayapata umeme kutokana na athari hizo pia kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao kwa uhakika na kwausalama pasipi madhara yeyote yale yatokanayo na umeme.

Pia Mhandisi Shamba amewataka wakazi wa jiji la Arusha kuondoa hofu juu ya shirika hilo la Tanesco na kuto kugusa nyaya za umeme zilizo anguka chini na kuwataka watoe taarifa mara moja pindi wainapo tofauti yeyote ya miundo mbinu ya umeme,(Tanesco inaangaza maisha yako).
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: