Wednesday, 4 September 2019

Rais Magufuli atangaza kuwasamehe January na Ngeleja kuhusu sauti zilizovuja


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa amewasamehe January Makamba na William Ngeleja baada ya kumkosea na kuomba radhi.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma zilivuja sauti kwenye mitandao ya kijamii za January Makamba na William Ngeleja ambazo zilimzungumzia Rais Magufuli kwa ubaya.

Baada ya ukimwa muda mrefu hatimaye leo Rais Magufuli amesema January na Ngeleja walimfuata na kumuomba radhi na aliwasamehe kwasababa alijua suala hilo likifika kwenye kamati ya chama litakuwa kubwa zaidi.

Ikumbukwe wakati suala hilo likiwa limeshika kasi kwenye mitandao ya kijamii ndipo Rais Magufuli alitengua uteuzi wa January Makamba ambaye alikuwa akitumikia wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipohudhuria Mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa Bodi ya Usajili wabunifu na Wakadiriaji Majenzi(AQRB), Bodi ya Usajili Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB) na Wadau wa Sekta ya Ujenzi  inayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a comment