Saturday, 28 September 2019

DK.BASHIRU AKABIDHI SHILINGI MILIONI MOJA KWA MFANYAKAZI BORA CCM MWAKA 2019


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Bashiru Ally Kakurwa, Leo, Amemkabidhi  Komredi Yohana Lukosi Anayefanya Kazi katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Yaliyopo Jijini Dodoma, Cheti cha Mfanyakazi Bora wa Chama Hicho kwa Mwaka Huu Pamoja na Kitita cha Fedha Shilingi Milioni Moja Ambapo Laki Tano Iliyotolewa na Chama Hicho na Laki Tano Nyingine Kuchangiwa na Viongozi Waliohudhuria katika Shughuli Fupi ya Makabidhiano ya Cheti Hicho.

Akizungumza Baada ya Kutoa Cheti cha Ufanyakazi Bora wa Mwaka 2019 iliyokwenda kwa Mfanyakazi Huyo,Katibu Mkuu wa CCM,Dk.Bashiru, Aliipongeza Kamati Maalumu ya Uangalizi wa Utendaji Kazi wa Wafanyakazi kwa Kumaliza Vizuri Mchakato Huo Ambapo Alisifia na Sifa na Vigezo Vilivyomsababishia Komredi Yohana Lukosi Kuwa Mshindi wa Mfanyakazi Bora kwa Mwaka Huu kwa CCM, Alisema Kwa Sifa Alizozipata za Utendaji Kazi wa Mtumishi Huyo wa Chama Alistahili Kupata Ushindi Huo na Kuwataka Watumishi Wengine Kuiga Mfano Wake.

“Sisi Sote Tumesikia Sifa Zilizofanya Mtumishi Mwenzetu Kushinda Kuwa Mfanyakazi Bora kwa Mwaka 2019 Tulipaswa Shughuli Hii Tuifanye Tangu Mei Mosi katika Sikukuu ya Wafanyakazi Ila Kutokana na Majukumu Yetu Tulipeleka Mbele Hatimaye Leo Tumemtunukia Mwenzetu Cheti cha Ufanyakazi Bora Pamoja na Sh.500,000 kutoka Chama na Mimi na Viongozi Wenzangu Hapa Mbele Tukamchangia Hadi Kufika Sh.Milioni Moja,Niwaombe Watumishi wenzangu Tuige Mfano wa Utendaji Kazi wa Komredi Yohana Lukosi;

“Yapo Mambo ya Muhimu yaliyoasisiwa na Tanu na Asp Ambayo Hadi Sasa CCM Lazima Tuyahifadhi Mfano kwa Kumbukumbu ya Ukumbi Huu Hata Kama Mchumi Wetu Anataka Fedha Hatuwezi Kuubadilisha Ukumbi Huu wa White House Kuwa Kumbi ya Starehe Eti Kisa Tunaingiza Fedha, Ila Kuna Mambo Ya Kubadilika Kulingana na Hali Ilivyo,Chama Chetu Kwa Sasa Tupo Vizuri Kiuchumi Hii Inatokana na Utendaji Kazi Wenu Ninyi Ndugu Zangu Watumishi” Alisema Katibu Mkuu, Dk.Bashiru.

Aidha Dk.Bashiru Aliwaambia Watumishi Hao Kujitoa kwa Moyo Wote katika Kuhakikisha CCM Kinafanya Vyema Utendaji Kazi Wake Ili Kiendelee Kushika Hatamu,Alisema Hata Kama Mfanyakazi Akilipwa Mshahara Mkubwa Ila Asipokuwa na Moyo wa Kujitolea Hakuna Kitakachoendelea kwa Hilo Nawapongeza Sana Wanachama Wenzangu wa CCM Tunazidi Kusonga Mbele na Kuzikabili Changamoto Zetu,Tuzidi Kufanya Kazi kwa Bidii Mabadiliko Yatakuja Tu Kama Si Leo Basi Kesho.

Pia Katibu Mkuu Huyo Aliwakumbusha Wanachama Hao Kujiendeleza katika Elimu Ikiwezekana Mfanyakazi Akajiendeleze Kulingana na Kazi Zao Akatolea Mfano Dereva wa Kawaida Akienda Kusomea Jinsi ya Kuendesha Viongozi (VIP) Itampa Ufahamu wa Namna Bora ya Utendaji Kazi Wake, Alitoa Maagizo kwa Chama na Jumuiya Zake Ziandae au Ziwasomeshe Watumishi Wake Kwa KUwa Elimu Haina Mwisho,Alitoa Mfano Akisema Ikitokea Dereva Akataka Kwenda Kufundishwa Kupika Chakula Kizuri Hatogharamia Kila Mtumishi wa CCM Ingependeza Asomee Kile Anachokifanyia Kazi.

Akitoa Salamu katika Mkutano Huo,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,Rodrick Mpogolo,Alimuambia Katibu Mkuu, Dk.Bashiru Kuwa Wamejipanga katika Kuhakikisha Chama Hicho Kinashinda kwa Asilimia 100% katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vitongoji na Vijiji Kutokana na Utekelezaji Mzuri wa Serikali ya Awamu ya Tano Inayotokana na Chama Hicho Inayosimamiwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais,Dk.John Pombe Joseph Magufuli.

Mkutano Huo Pia Ulihudhuriwa na Makatibu Wakuu wa Jumuiya Zote za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ambao ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania,Erasto Sima,Katibu Mkuu Uvccm,Mwalimu Raymond Mwangala,Katibu Mkuu wa UWT,Mwalimu Queen Mlozi na Viongozi Wengine.

Mwishoo 

0719976633.

No comments:

Post a comment