MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifungua kikao cha kamati ya afya ya msingi wilaya hiyo kuhusu mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kilichofanyika mjini humo iliyokwenda sambamba na uhamasishaji wa kunywa dawa za kukabiliana na magonjwa hayo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wilayani humo kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza Dkt Flora Kessy akifuatiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Nassoro Moyo 
Msimamizi wa zoezi la Kinga Tiba katika ngazi ya Jamii kutoka wizara ya Afya Fadhili Katula akizungumza wakati wa kikao hicho

Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilaya ya Muheza Julius Mgeni  akisisitiza jambo kwenye kikao hicho
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo

 Sehemu ya wataalamu waliohudhuria kikao hicho
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza Bakari Mhando kulia akiwa na Diwani wakifuatilia kikao hicho
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akipima urefu kabla ya kuanza kutumia dawa
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Bakari Mhando kushoto akipatiwa dawa



MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha kwamba wanapotoa dawa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa usubi kwenye maeneo yao wahakikisha wanaziweka maeneo salama ili kuepusha kuwafikia walaji ikiwa imepoteza ubora wake.

Mhandisi Mwanasha aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi wilaya hiyo kuhusu mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kilichofanyika mjini humo iliyokwenda sambamba na uhamasishaji wa kunywa dawa za kukabiliana na magonjwa hayo kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri wilayani humo.

Alisema kwamba changamoto kubwa ya watoa dawa wengine wanawapelekea wanafamilia huku akiwataka watumie utaratibu wa mikutano ya hadhara ikiwemo kuwataka wasiwaachie viongozi wa vitongoji kuteuwa watu wenyewe bali mikutano ianze ili kutolewa elimu kwa wananchi wote waelewa manufaa ya kunywa dawa na madhara ya kuwa na ugonjwa huo ndio watatoa ushirikiano wa kunywa dawa hizo.

“Kwani wakipatiwa elimu ya manufaa ya kunywa dawa hizo na madhara yanayoweza kuwakumba iwapo hawatakunywa itakuwa chachu ya wananchi wengi kuweza kujitokeza pia tumeambiwa magonjwa hayo yanaambukizwa na mbu,inzi lakini mbu hatuwezi kumtokomeza kama hatufanyi usafi tusienda tu kuhamaissha suala la kumeza dawa lakini tuhamasishe suala la usafi wa mazingira”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba ili kuweza kuondoa mazalia ya mbu kwenye maeneo yao lazima yawe safi na salama huku akieleza namna suala la usafi lilivyokuwa jambo muhimu mpaka Rais Dkt John Magufuli aliweka siku mahususi kwa ajili ya watu kufanya usafi.



Aidha alisema hiyo inaonyesha namna serikali inavyotaka maeneo yao yawe masafi hivyo tuhamasisha wananchi kuhakikisha wanakula dawa hizo ili kuweza kuondokana na suala hilo.



“Labda niwaambia kwamba hizi zote ni juhudi za CCM tunajua Serikali inaongozwa na CCM ni kutaka wananchi kuwa na afya njema kwa lengo la kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo “Alisema

Awali akizungumza kwenye kikao hicho Msimamizi wa zoezi la Kinga Tiba katika ngazi ya Jamii kutoka wizara ya Afya Fadhili Katula alisema kwamba hapa muheza wanafanya kwenye suala la tatizo la Usubi hiyo ni wilaya Kongwe ambayo imekuwa ikitoa dawa kwa miaka iliyopita mpaka sasa wanaendelea na juhudi hizo.



Alisema kwamba wanaendelea kuhamasisha lengo kufikia kiwango cha chini kwa kutokomeza kabisa usubi kwa hiyo nia pekee ni kumezesha dawa kwenye jamii ili kufikia kila mwananchi anapata dawa ili kuweza kuzuia na kumtibu kama anavimelea.



Alisema wanapambana lengo lao asilimia kuanzia 85 na kuendelea wawe wamemeza dawa ili m wisho wa siku wilaya hiyo isahau kuhusu ugonjwa huo na kuelekeza nguvu kwenye magonjwa mengine





Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza (DMO) Dkt Flora Kessy alisema kwamba ugonjwa wa Usubi upo kwenye wilaya hiyo hivyo wao kwa kushirikaana na wizara ya Afya na wadau wengine wameendelea kuwekeza kwenye idara ya afya ili kutokomeza au kupunguza kwa kiasi kikubwa janga hilo.



Dkt Flora alisema wanapambana kwa kiasi kikubwa kuweza kuhakikisha unamalizika kwani madhara yake ni makubwa na zaidi ni kusababisha upofu kwa watu ambao wanakabiliwa nao jambo ambalo limewafanya kuanza kuchukua hatua za makusudi kukabiliana nao



“Kwani mwananchi anapopata upofu shughuli za uendelezaji wa maendeleo ya nchi haupo tena anakuwa tegemezi kwa nchi na jamii inayomzunguka na ndio maana tumeamua kuanza kukabiliana na tatizo hilo kwa vitendo “Alisema Dkt Flora.



Naye kwa upande wake Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele wilaya ya Muheza Julius Mgeni alisema kwamba hivi wanakusanya silaha kwa ajili ya kugawa dawa za usubi kwa wananchi ili kuweza kujikinga na magonjwa hayo.



Alisema kwenye wilaya yao walianza utekelezaji wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele miaka kumi na tisa iliyopita tokea 2000 wakiwa na mpango maalumu wa kutokomeza ugonjwa wa usubi.



Alisema lakini mwaka mwengine 2004/2005 wakaanza kutekeleza mpango wa kutokomeza magonjwa ya mabusa na matende baadae waliunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza hilo.

Mwisho.


Share To:

Post A Comment: