Wednesday, 4 September 2019

BREAKING: Ndege ya Air Tanzania Iliyokuwa Inashikiliwa Afrika Kusini Yaachiwa Huru

Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja na mlalamikaji alipe gharama za kesi.

Kwa sasa, mchakato ya kuichilia ndege hiyo kurejea nchini  ikitokea katika uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg inaendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo  huko mahakamani amesema kuwa Tanzaia imeridhishwa na uamuzi wa mahakama.

No comments:

Post a comment