Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifungua  mkutano wa 53 wa utabiri wa msimu wa vuli kwa nchi 11 za pembe ya Afrika unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Hayat Regency jijini Dar es salaam leo.
Meza Kuu
SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) nchini, kutoa taarifa na tahadhari za mapema za hali ya hewa kwa vile ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu ya kijamii na uchumi katika nchi zetu na ukanda wote Wa pembe ya Afrika

Waziri Wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasikiano Mhandisi Izack Kamwelwe amezungumza hayo leo jijini Dar es Salaam alipofungua mkutano wa 53 wa utoaji wa utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa mvua za vuli kwa nchi 11 za pembe ya Afrika.

Mhandisi Kamwelwe amesema ni vema utabiri ukatolewa kwa wakati sababu nchi nyingi za ukanda huo ikiwemo Tanzania zinategemea sana hali ya hewa.
"Sekta Kama vile kilimo na usalama wa chakula, maji, Nishati, Afya, Mifugo, uvuvi na shughuli nyinginezo zinazofanyika baharini, usafirishaji na utalii na nyingine nyingi hutegemea sana hali hewa hivyo mabadiliko ya hali hewa yanayoambatana na vipindi virefu vya ukame na mvua yanaendelea kuufanya utabiri kuwa Wa umuhimu sana..
Aidha, Kamwele ameshauri kutumia pia njia za asili za kutabiri hali ya hewa kuliko kuachana nazo kabisa huku akisisitiza kwamba njia hizo zinaweza kuboreshwa.
"Hata wakati wa kubadili sheria kutoka kwenye Agency kwenda kwenye Authority tulipata ushauri kwamba hata kakakuona tunaweza kumtumia kuandaa utabiri," alisisitiza Waziri Kamwelwe.
Waziri huyo aliwataka washiriki 200 wa mkutano huo watatoka na maazimio yatakayochangia upatikanaji wa taarifa sahihi zaidi za hali ya hewa ili kuwasaidia watumiaji wa taarifa hizo kwenye shughuli zao za maendeleo kwa nchi shiriki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi amesema wataalam hao pamoja na kujadiliana na kukubaliana na kufikia muafaka Wa pamoja juu ya utabiri wa hali ya hewa wa msimu ujao wa mvua za vuli Oktoba hadi Desemba watatoka na utabiri wa nchi wanachama kwa maendeleo ya nchi zao.
"Hii ni mikutano inayofanya mara kwa mara kabla ya kuandaa taarifa ya msimu kwenye nchi zetu huwa tunakutana na kutoa utabiri wa ukanda wetu huu na mwaka huu kauli mbiu yake ni utoaji wa tahadhari kwa hatua za haraka katika kukabiliana na athari za hali mbaya ya hewa.
"...Naamini mkutano huu utakuwa na matokeo chanya hivyo basi watumiaji wa taarifa zetu waendelee kusubiri," alisema Dk. Kijazi huku akifurahia Tanzania kupewa heshma ya kuandaa mkutano huo muhimu Afrika.
Amesema ingawa kuna changamoto kubwa upungufu wa hali ya hewa, Tanzania imejenga miuondombinu ya hali ya hewa ikiwemo kujenga rada na tayari mpaka sasa kina rada mbili na Tatu ziko katika hatua ya manunuzi ambapo mpango wa TMA ni kuwa na rada saba.
Akizungumzia mvua zinazoendele kunyesha, dk. Kijazi amesema kuwa zipo nje ya msimu huku akibainisha kwamba ni mabadiliko yanayosababisha kupungua kwa mkandamizo wa hewa baharini jambo linalosababisha unyevu kwenye anga.
"Sio mvua kubwa na hazitachukua muda mrefu, hizi zipo hasa ukanda wa Pwani na mikoa inayozunguka Ziwa Victoria... Wananchi wasihofu," alisema Dk. Kijazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TMA, Burhani Nyanzi alisema mkutano huo unalenga kuwasaidia watu wote wanaofanya shughuli zao wakitegemea hali ya hewa.

Kongamano hilo linahusisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka nchi mbali mbali zikiwemo, Tanzania, Ethiopia, Sudan, Sudan ya kusini Burundi, Djibouti, Elitrea, Kenya, Somalia, Uganda nw Rwanda.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: