Wednesday, 28 August 2019

MBUNGE AKUNWA KWA UTENDAJI KAZI WA MKURUGENZI WA WILAYA IKUNGI


Na Dotto Mwaibale, Dodoma.

MBUNGE wa Singida Magharibi,  Elibariki Kingu (pichani) amekunwa na kupongeza jitihada za maendeleo zinazofanywa na Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Justice Lawrance Kijazi katika wilaya hiyo.

Kingu alitoa pongezi hizo jijini hapa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakatiakitoa taarifa ya maendeleo ya jimbo lake.

"Katika jimbo langu tumetekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Vituo vya afya, madarasa na miradi mikubwa ya maji na haya yote tunayakamilisha kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wetu  Kijazi"

Alisema  uzalendo unaooneshwa na Mkurugenzi huyo  katika kusimamia miradi ni wa kuigwa katika taifa .,nimekua Dc najua nimekaa  na wakurugenzji huyu kijana hakika uzalendo wake katika kazi ni wa kutukuka katika wilaya yetu.

" Kijazi ameunganisha Halmashauri yetu katika kusimamia miradi mbalimbali ,Mfano mradi wa kituo cha afya Sepuka kwani tulipewa na Serikali sh. milioni 400 ambapo ujenzi wake ni wa kiwango cha juu na hapo ndipo utajua huyu kijana ni hazina kwa nchi,sijawahi kumsifia mkurugenzi hadharani" alisema Kingu.


Aliongeza kuwa ili halmashauri zetu ziweze kuwa na maendeleo kunahitajika kuwepo na ushirikiano mkubwa kwa viongozi wa wilaya husika kuanzia wakuu wa wilaya, wakurugenzi, madiwani, wabunge na wataalamu mbalimbali.

Kingu alisema kila mtu mwenye uzalendo wa nchi hii ana wajibu wa kushirikiana na viongozi kuanzia ngazi ya vijiji hadi Taifa katika kuiletea nchi yetu maendeleo.

No comments:

Post a comment