Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo leo hii Agoust 16 amemaliza mgogoro wa wanafunzi uliokuwa umeota sura mbaya ya kuhatarisha hali ya amani shuleni hapo ambapo mgogoro huo ulianza tangu Augost 10 mwaka huu. 

Waziri huyo wa TAMISEMI alitoa onyo kwa walimu ambao inaonekana wameshindwa majukumu yao ya kiuongozi hadi shule kuingia katika mapigano makubwa kati ya kidato cha tano na kidato cha sita pamoja na  kuchipuka kwa tofauti za mitazamo ya kidini shuleni hapo.

Wanafunzi na walimu wa shule hiyo wamemshukuru sana waziri huyo kwani walikiri kwamba uhasama shuleni hapo ulikuwa mkubwa sana.

Waziri huyo alifanikiwa kuongea na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa pamoja na kamati ya Wilaya ya Moshi,Bodi ya shule wakiwa pamoja na walimu wote wa shule hiyo, na kuhitimisha na kikao cha wanafunzi.

Jafo alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mgwira kuendelea kufanya uchunguzi wa waanzilishi wa chokochoko hizo ili watakao bainika wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Aidha,Jafo alimaliza ziara hiyo shuleni hapo kwa kuunda timu kumi zenye mchanganyiko mbalimbali ambazo zitashindana katika michezo mbalimbali na kuzipa majina ya Tanzanite,Gold,Diamond,Kilimanjaro, Manyara,Serengeti,Ngorongoro,Mikumi, Nyerere Park, na Ruaha kitendo ambacho kilisababisha shangwe kubwa kwa wanafunzi hao
Share To:

msumbanews

Post A Comment: