Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi
wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza
Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo
eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.(Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu
ya washiriki wakifatilia kwa karibu hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya
kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi
nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo eneo la Kisasa,
Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Bi
Gloria Emmanuel ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi Wilayani Monduli
wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna
bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa
St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Shaban
Minja ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi Wilayani Same wakati wa
ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya
kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St.
Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Mwenyekiti
wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud
Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini akizungumza wakati
wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya
kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St.
Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi
wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza
Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa St. Gasper uliopo
eneo la Kisasa, Jijini Dodoma leo tarehe 3 julai 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Jitihada
za kuongeza uzalishaji zinakuwa na mafanikio hafifu kutokana na
kutotumia teknolojia sahihi zinazoendana na mahitaji na wakati;
Mathalani, matumizi ya zana za kulimia ama zikiwa za mkono au
zinazokokotwa na wanyamakazi au matrekta, zimekuwa zikisababisha
mmomonyoko wa udongo hasa katika maeneo yasiyo tambarare na kusababisha
upotevu mkubwa wa rutuba na kujengeka kwa jasi (hard pan).
Kwenye
maeneo yenye mvua chache njia hizo za kilimo cha kukatua ardhi
hazitunzi unyevu na kusababisha uzalishaji kuwa wa chini hasa pale
panapokuwa na vipindi virefu vya ukame (dry spells) kama ilivyotokea msimu huu wa kilimo katika baadhi ya maeneo nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 03 julai
2019 kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna
bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika katika ukumbi wa
St. Gasper uliopo eneo la Kisasa, Jijini Dodoma.
Mhe
Hasunga anasema kuwa kwa sababu hiyo basi, ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi ni muhimu kubadilisha mifumo inayotumiwa katika
kuandaa mashamba ili kupata matokeo mazuri.
Amewashukuru Washirika wa Maendeleo (Development Partners)
pamoja na Wadau wote wa Kilimo Hifadhi waliowezesha kufanikisha warsha
hiyo muhimu wakiwemo African Conservation Tillage Network (ACTN),
Canadian Food GrainBank (CFGB), Diocese of Central Tanganyika (DCT), na
Conservation Farming Unit (CFU) –Tanzania.
Alisema
juhudi hizo wanazofanya za kuendeleza Kilimo Hifadhi kwa kushirikiana
na Serikali kwa maendeleo ya wakulima na Taifa kwa ujumla, ni sehemu ya
mwelekeo wa kufikia Uchumi wa Viwanda kwa kukuza uzalishaji wenye tija.
Aliongeza
kuwa jitihada hizo zinaendana na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013 na
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme - ASDP II) ambazo
zinahimiza usimamizi endelevu wa matumizi bora ya maji na ardhi,
kuongeza tija na faida katika uzalishaji, biashara na kuongeza thamani
ya mazao na kuiwezesha Sekta katika uratibu, ufuatiliaji na tathmini.
Kadhalika
Waziri Hasunga amesema kuwa ili kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo,
Serikali imeongeza juhudi za kuwaunganisha wakulima na masoko, huduma za
kifedha, usindikaji wa mazao na kuongeza thamani.
Alisema
kuwa katika kutimiza azma hiyo, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa
Kilimo inaendelea Kuweka mazingira mazuri yanayovutia uzalishaji na
uwekezaji, Kuimarisha mafunzo, Utafiti, ubunifu na uenezaji wa
teknolojia za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na Kilimo Hifadhi na
kuboresha Huduma za Ugani, Kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo,
uongezaji thamani ya mazao, kuimarisha ushirika, kuwaunganisha wakulima
na masoko na huduma za fedha; na Kuhamasisha na kusimamia matumizi ya
teknolojia za kisasa za kilimo ikiwemo teknolojia za kilimo hifadhi kwa
kushirikiana na wadau mbali mbali.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo
na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa (Mb) alisema kuwa serikali inapaswa
kujipanga vizuri kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini kwa kufanya utafiti wa
kina kwa utafiti ndio nguzo ya kilimo.
Alisema
kuwa asilimia kubwa ya mbegu zinaagizwa nje ya nchi hivyo aliiomba
aserikali kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo hususani katika kuendeleza
sekta ya mbegu.
Amesema
Tanzania bado kuna tatizo kubwa la Masoko kwani wakulima wengi
wanazalisha mazao yao lakini hawana mahali pakuyauza kwa bei nzuri huku
wengine wakishindwa kusafirisha mzao yao kutokana na miundombinu
kutoimarika kwa kiasi kikubwa. Kadhalika ameipongeza wizara ya Kilimo
kwa kuanzisha mchakato wa mapitio ya sera ya kilimo ya 56mwaka 2013
itakayopelekea kuwa na sheria mpya ya Kilimo.
Awali
akitoa salamu za wizara ya Kilimo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kufungua warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew
Mtigumwe alisema kuwa Lengo
la warsha hiyo ni kuwawezesha washiriki kupata uzoefu na kufahamu
juhudi na matokeo ya kazi za kuendeleza kilimo hifadhi zinazofanyika
nchini na kuweka mpango utakounganisha, kuratibu na kusimamia shughuli
za kuendeleza matumizi bora na endelevu za teknolojia za kilimo hifadhi
nchini.
Alisema kuwa matumizi ya kilimo cha kisasa (smart agriculture) ikiwa
ni pamoja na kilimo hifadhi ni nguzo katika kuendeleza kilimo nchini
kwa kongeza tija, kuboresha ardhi na kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi hasa katika maeneo yanayopata mvua chache.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka. Tathmini
zilizofanywa na Wizara zinaonyesha kuwa karibu hekta 40,000 nchini
zinalimwa kwa kutumia kilimo hifadhi na matokeo yanaonyesha kuwa
mavuno (yields) wanayopata wakulima kutoka kwenye mashamba ya kilimo hifadhi ni mazuri hata wakati wa mvua chache.
Aliongeza
kuwa Katika kipindi hiki, ambacho Serikali inajitahidi kuongeza miundo
mbinu ya umwagiliaji na kuongeza matumizi ya mbolea za viwandani kwa
gharama kubwa ili kuongeza tija na kukabiliana na athari za mabadiliko
ya tabia nchi, matumizi ya teknolojia ya kilimo hifadhi ni njia mbadala
ya kufikia malengo hayo kwa haraka na kwa gharama nafuu.
MWISHO
Post A Comment: