Na.Vero Ignatus,Dar.

Miili ya wafanyakazi 5 wa Kampuni ya Azam Media waliopata ajali katika eneo la Kisonzo katikati ya eneo la Igunga (Tabora) na Shelui (Singida)imeagwa leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na  Waandishi wa hanari wa vyombo mbalimbali,Viongozi wa Serikali,viongozi wa vyama vya siasa,Dini na wananchi kwa ujumla.

 Akitoa salam za rambirambi katika msiba huo mzito ulilolikumba Taifa ,Waziri wa Habari,Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Harison Mwakyembe amekemea tabia ya baadhi ya watanzania wanaopiga picha kajali inapotokea na kuzirusha kweye mitandao ya kijamii ambapo amesema Serikali imetoa onyo la mwisho na haitalisemea tena.

Dkt.Mwakyembe amewataka   Watanzania kuwa na utu bila kushurutishwa  na sheria kwani Sheria ya makosa ya mtandao hairuhusu jambo kama hilo kwani hakuna faida yeyote anayoipata mtu kwa kupiga picha za miili ya watu waliokufa.

"Hebu tuendeleze utamaduni na utu bila kushurutishwa na sheria ,acheni tabia ya kurisha picha za watu waliofariki kwenye ajali na kurusha kwenye mitandao,sheria ya makosa ya mitandao inakataza tutakufunga,hili ni onyo la mwisho hatutasema tena kuanzia hapa"akisisitiza Mwakyembe.

Hamad Masauni ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kampuni ya Azam imekua ikishirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kutoa elimu kuhusiana na maswala ya usalama na watumiaji.wa barabara.

"Sisi ni miongoni mwa waathirika wakubwa kutikana na kuondokewa na vijana hawa"
Jeshi la polisi tayari limeshaanza uchunguzi kuhusiana na  ajali hiii na uchunguzi huo unaendelea vizuri na tayari tumeshamkamata dereva wa lori aliyesababisha ajali"Amesema Masauni

Mhe.Masauni ametoa wito kwa watumiaji wa barabara kuendelea kuwa watiifu na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwani jeshi la polisi litaendelea kusimamia sheria za usalama barabarani siyo kwa nia ya kumkomesha yeyote bali kwa kuokoa maisha ya Watanzania.

Mhandisi James Kilaba ni Mkurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania
(TCRA) amesema wao kama wadau wa habari wanaifahamu michango mikubwa ya vijana hao kwani hata wiki iliyopita walikuwa wakifanya nao kazi hivyo ameitaka Azam Media kutokukata tamaa bali waendelee kufanya kazi maana hiyo ni safari ya wote.

Kwa upande wake msemaji muwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) umesema wameupokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa ambapo waliokatishwa maisha ni vijana na hiyo ni changamoto isiyoepukika kwa ni ratiba ya kila mwanadamu kupitia njia ya kifo.

Mwenyekiti wa Baraza la Wahariri nchini Nevil Meena aliyewakilishwa ndugu Balile amesema matukio hayo yanamkumbusha  kila mmoja kukesha maana hatujui kwani hakuna ajuae siku wala saa ya kuondoka duniani huku akisisitiza madereva kuzingatia kuwa mwendo kasi unaua,unaleta hasara ,kwa masikitiko makubwa  kwa Taifa.

Rose Ruben ckutoka Tamwa amesema wamekuwa mstari wa mbele na wadau  wakubwa wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani  na kuepuka ajali za kujitakia

"Athari ya kuwapoteza vijana hawa hatutaiona leo ila baada ya miaka 20 ndipo itaonekana kwani vijana hawa wabgeliwafundisha wengine kazi na wakazaliwa watendaji wengi zaidi hii ni huzuni kubwa "alisema

 Amewasihi watumiaji wa barabara kuwa makini wakichukua taharhari kubwa kwani ajali zinapoteza nguvu kazi ya Taifa,zinaleta Ulemavu wa kudumu ,na vifo visivyotarajiwa.

Tanzania,tumepoteza vijana kwenye kazi chombo cha habari hakipelekwi kama hawana umahiri na usahihi,katika kazi za utangazaji hatuna wataalam wa kutosha na ni pigo kubwa,waandishi waliobakia wawaenzi vijana hawa ili tasnia iendekee kukua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Telebisheni ya Taifa Ndugu Rhioba ametoa pole kwa Azam Media huku akisema Vijana hao waliopoteza maisha kuna nyakati walisharusha matangazo yaliyonufaisha TBC hivyo Taifa limepoteza nguvu kazi .

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo mchini Haikael Mbowe amewaomba wale wote wanaomiliki vyombo vya habari wasiruhusu vyombo hivyo kuwagawa naomba  badala yake watumieni vyombo hivyo kwa weledi na kwa ulinganifu.

Tido Mhando ni Afisa mtendaji mkuu wa Azam media akitoa neno la shukrani salamu za rambirambi amewashukuru watanzania na wanahabari kwa kuwapatia lugha ya  faraja kwani walipata taarifa hizo za msiba kutoka kwa wasamaria wema walioona ajali hiyo.

Amesema kwenye gari hiyo walikuwepo wafanyakazi 8 walikuwa wakielekea Chato kwenye kazi ya uzinduzi ilikuwa ifanyike leo kwani wamekuwa wakipata mialiko mingi za kazi za Kitaifa. 

Amesema  wafanyakazi hao walikuwa wapo safarini kutoka Dar es salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Bugiri -Chato kwaajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hiyo leo.

Majina ya waliopoteza maisha yao ni pamoja na Charles Wandwi (1980)Florence Bitaliho Ndibalema (1989)Said Haji Hassan (1989)Salum Juma Mhando (1985) Silvanus Waziri Kassongo.(1989)

Mwisho.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: