Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sophia Mjema  akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya Wadau wa Uwekezaji Dar es Salaam

NA HERI SHAABAN

SERIKALI imekiagiza kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC ) iwapambanishe Wawekezaji kila Wilaya kwa manufaa ya Taifa letu.


Hayo yalisemwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sophia Mjema ,wakati wa ufunguzi wa warsha ya Wadau wa Uwekezaji Dar es Salaam.

" Watanzania tubadilike ili twende katika mapinduzi ya Uchumi wa Viwanda naomba kila wilaya muweke utaratibu wa kuwapambanisha wawekezaji kwa ajili ya manufaa ya Taifa " alisema Mjema.

Mjema alisema katika mkoa wa Dar es Salaam jiji linaloongoza kwa biashara kama njia kuu ya uchumi ambapo inachukua takribani asilimia 80 ya shughuli zote za kiuchumi za wakazi wa mkoa huo kuwa ni biashara.

Aidha alisema nusu ya miradi ya uwekezaji hapa nchini ipo katika mkoa wa Dar es Salaam hivyo zairi kuwa uboreshaji wa mazingira ya biashara ni jambo muhimu sana...


Alisema asilimia 80 ya shughuli zote za kiuchumi za wakazi wa mkoa huo ni biashara na nusu ya miradi ya uwekezaji ipo Dar es Salaam,hivyo uboreshaji wa mazingira ya biashara ni jambo muhimu .

Mjema alisema warsha hiyo pia itajadili changamoto mbalimbali zinazochangia uwepo wa mazingira magumu ya ufanyaji wa biashara hapa nchini yanayohusisha maeneo ya sera ,sheria ,miongozo,kodi,tozo, pia mtajadili usajili wa biashara ,vibali leseni za ukaguzi , aliwataka wazingatie na kuvipa uzito wa kipee.

Aliwataka watumie fursa hiyo kujadili kwa kina masuala yote kama yalivyopangwa huku wakiangalia masuala ya uwekezaji kwa kupitia Taasisi ya Uwekezaji Tanzania TIC ili muweze kutoka na maazimio mahsusi yatakayoboresha ama kupelekea uboreshaji wa mazingira ya biashara katika ngazi ya mkoa.

"Serikali ya awamu ya tano imedhamilia kuimalisha uchumi na kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwanzishwaji wa viwanda na kwa kuwa Dar es Salaam ni kitovu cha biashara Tanzania ni vyema sasa tuone umuhimu wa kuwa na mazingira bora kabisa ya kibiashara kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi na hivyo kufanya washiriki mahususi wa maono ya kiongozi wetu Rais John Magufuli ya Tanzania ya viwanda" alisema

Kwa upande wake Meneja wa Kanda Mashariki TIC Venance Mashiba alisema dhumuni la warsha hiyo kujipanga katika kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano kukuza uwekezaji kwa ujumla Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Mashiba alisema katika uwekezaji pia kuna changamoto mbalimbali masuala ya udhibiti wa kifedha ambayo pia yanaitaji maboresho katika masuala ya vibali,leseni na ukaguzi changamoto hizo zimetajwa kwenye uchambuzi uliofanywa na serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara .

" Katika jiji la Mkoa wa Dar es Salaam changamoto nyingine ni pamoja na ukosefu wa maeneo yaliotengwa kwa ajili ya uwekezaji,migogoro ya ardhi,miundombinu duni,upatikanaji wa maji na umeme baadhi ya maeneo ,misururu ya magari na uhaba wa maegesho" alisema Mashiba.

Mwisho
Arnatogluo
Juni 27/2019
Share To:

Post A Comment: