Na Woinde Shizza,Arushqa

waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu  uwekezaji Angela Kairuki ameeleza kuwa Serikali itatumia watalii wanaokuja kutembelea vivutio vyetu kutangaza fursa  zilizopo Za uwekezaji katika sekta ya italii ,biashara pamoja na madini. 


Angela Ameyasema hayo wakati akizungumza na wawekezaji kutoka nchini China Jana katika kituo cha mikutano AICC kilichopo ndani ya jiji la Arusha ambapo alisema lengo la mkutano huo nikubadilishana mawazo na uzoefu katika eneo la uwekezaji pamoja na kutangaza fursa za kibiashara ambapo alibainisha kuwa serikali tukufu ya John Pombe Magufuli ipo bega kwa bega na serikali ya china kujenga jamii yenye ushirikiano na maendeleo. 

Alisemakuwa wanakaribisha maamuzi ya china kufungua milango kwa Tanzania katika kuwekeza katika mpango mmoja kuweza kulifikia soko Lake kubwa Katika sekta zote muhimu kuanzia katika uwekezaji upande wa utalii, biashara, madini na Fedha.

"napenda kuwahakikishia marafikizangu WA China kuwa Tanzania ni ya amani unapokuja kuwekeza Tanzania uwenauhakika wa usalama wako binafsi, pia tupo tayari kukaribisha uwekezaji kutoka china na kuwahakikishia usalama wa mitaji yenu Kwani tunazosera nzuri na sheria thabiti. "alisema Kairuki. 

Alibainisha kuwa Tanzania ni mshirika anaetegemeka  na mdau anae aminika kwa china hivyo ndio sababu haikua ajali kwa nchi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza za Afrika kuhusishwa Katika mpango wa ukanda mmoja wa kibiashara (one belt One road initiative) kwa sababu hiyohiyo Nchi yetu ni miongoni mwa nchi nne vinara chini ya mpango wa uzalishaji na uwezeshaji wa pamoja wa china. 

amewataka watanzania kuitangaza vizuri nchi hususani ni kipindi hichi watalii wanakuja kutembelea vivutio vyetu huku akiwataka waandishi wa habari kwa kuona umuhimu wa kuitangaza nchi yao kama vile waandishi kutoka nchini China wanavyofanya. 



Nae naibu waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu sera uratibu bunge kazi na ajira na watu wenye ulemavu ANTHONY MAVUNDE amesema serikali inapenda wageni na wafanyakazi kutoka nje ya nchi kwa kuwa wanasaidia kuongeza ujuzi ila wawapo nchini wanaitajika kufuata sheria



Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffey  Mwambe alisema  kuwa kongamano hilo litasaidia ukuaji wa uchumi na wao wamejipanga kikamilifu kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo  nchini ambazo  sasa zimefunguka kwa wingi.

Jumla ya wawekezaji 50 kutoka makampuni 25 wameweza kushiriki kongamano hilo ambapo pia wageni hao kutoka taifa la watu wa China 336 watapata fursa ya kutembelea vivutio vya  utalii ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro.

picha ikionyesha 40 Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu  uwekezaji Angela Kairuki akiongea na waandishi mara baada ya kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini China



picha ikionyesha 49 naibu waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu sera uratibu bunge kazi na ajira na watu wenye ulemavu ANTHONY MAVUNDE akichangia jambo katika mkutano huo

picha ikionyesha 54 mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Geoffey  Mwambe akiongea katika mkutano
Share To:

msumbanews

Post A Comment: