Wednesday, 1 May 2019

RC Makonda aagiza wafanyakazi Dar kupandishwa madarajaMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuagiza Katibu tawala wa Mkoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanawapandisha madaraja Watumishi wanaostahili ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.

RC Makonda ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambapo amesema kinachomshangaza ni kuona wafanyakazi wanaostahili kupandishwa madaraja hawapandishwi licha ya kuwa na sifa na vigezo vinavyostahili.

Aidha RC Makonda amewaagiza maafisa kazi kushughulikia kero za wafanyakazi kwa wakati ili watumishi wafanye kazi zao bila vikwazo.

No comments:

Post a Comment