Friday, 3 May 2019

Nyota wanne wa Simba SC kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Mbeya CityNyota wanne wa kikosi cha Simba SC kesho wataukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya majira ya saa 10:00.

Ofisa Habari wa Simba SC, Haji Manara amesema kuwa watawakosa wachezaji wao wanne kutokana na kutokuwa fiti kiafya.

"Tutamkosa John Bocco, ambaye aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania, alishindwa kumaliza dakika 90, Asante Kwasi aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya Biashara United, Pascal Wawa aliumia kwenye mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe na Shomari Kapombe.

"Wachezaji wote kwa sasa wanaendelea vizuri, tayari Kapombe na Wawa wameanza mazoezi yao binafsi ya gym ili kujiweka fiti, mashabiki waendelee kutuombea dua tufanye vizuri," amesema Manara.

No comments:

Post a Comment