Tuesday, 7 May 2019

DC Mjema agawa vyakula kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

MKUU Wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema, amegawa vyakula kwa watu wasio na uwezo ili kuweza kuwasaidia katika mfungo wa Mwezi Wa Ramdhani.

Tukio hilo la  ugawaji vyakula limefanyika leo Ofisini  kwake kufuatia Shirika la  ISTIQAMA COMMUNITY kumuunga mkono DC Mjema kwa ajili ya kuwasaidia wale wasio na uwezo .

Akizungumza na Waandishi Wa Habari, DC Mjema, amesema Ofisi yake imekuwa na utaratibu Wa kugawa vyakula kila ifikapo kipindi cha Mwezi mtukufu Wa Ramadhani.

Amesema mbali na Ofisi yake pia kuna kuwa  na wadau mbali mbali wanaojitokeza kuungana na Ofisi yake kwa ajili ya zoezi hilo. Amemshukuru Katibu Mtendaji wa  ISTIQAMA COMMUNITY TANZANIA , Sheikh Seifu Salumu kwa kusaidia kutoa Tende  na Sukari jambo ambalo limeongeza kuwafikia watu wengi na kuitakia kheri Shirika  hilo wazidi kufanikiwa.

Amesema miongoni Mwa vyakula vilivyotolewa na ISTIQAMA COMMUNITY ni pamoja na Sukari Kilo 300 na Tende  Kilo 168. Amesema Ofisi yake imegawa Mchele, Sukari, Mafuta ya kula, Maharage pamoja na Tambi.

" Huu ni Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani tunagawa vyakula hivi sio kwa watu wote Bali ni kwa wale wasio na uwezo ili wafunge funga  zao vizuri na kwa utulivu " Amesema DC Mjema..

 Pia amewataka Waislamu kukitumia kipindi hiki kifupi kama njia ya kuomba toba kwa Mola na kuomba mazuri yote  na kuombea wagonjwa, familia , Viongozi Wa Kitaifa ili wafanikishe Yale wanayotaka kulipeleka Taifa hili mbele zaidi kufikia uchumi Wa kati.

Amesema hiki ni kipindi kizuri kwahiyo wakitumie vizuri na mambo makubwa na faida wataziona maana ni moja ya nguzo za imani katika Uislamu.

Ameziomba na zile taasisi nyingine zenye uwezo ziweze kuwasaidia wale masikini maana kuna watu wanafunga lakini hawajui futari watapata wapi.

 Naye Katibu Wa ISTIQAMA COMMUNITY TZ , Sheikh Seif Salumu, amemshuru DC Mjema kwa kuwa  karibu  sana na Wananchi wake jambo ambalo linatia matumaini.

 Pia amewaomba Waislamu kuitumikia nafasi hiyo muhimu ili kupata Afya njema na swawabu nyingi  kutoa kwa Mwenyezi Mungu.

Amesema Shirika lao pia limefarijika kupokea wito katika Ofisi ya Mkuu Wa Wilaya na kuahidi ushirikiano mwema katika Maendeleo ya Wananchi.

No comments:

Post a comment