Maneno hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu ndg kamana juma Simba  alipokua akizungumza na Viongozi pamoja na Wanachama wa Umoja wa Vijana kutoka katika matawi ya Vyuo na vyuo vikuu mkoani Arusha

Khamana alisema"Umoja wa Vijana ni chombo mathubuti kilichoundwa ili kuwasaidia Vijana kwa kuyasemea na kuzi simamia Changamoto mbalimbali zinazowakabili Vijana wote nchini lakini pia ndio tanuru kuu la kuwaoka Viongozi wa leo na kesho katika Taifa letu"

Ndg Khamana amewataka Viongozi hao na Wanachama Kuendelea kusoma kwa bidii ili kuendelea kutengeneza wataalam Mbali mbali wazalendo wenye mapenzi mema na taifa letu walio pikwa na tanuru la kuokea Viongozi ili kuendelea kuisadia Serikali katika kushughulika na kutatua changamoto mbali mbali katika jamii zinazo tuzunguka

Alisema"Tusomeni kwa Bidii ili Taifa liendelee kupokea wataalam mbali mbali Wenye uzalendo na mapenzi mema katika Taifa letu waliopikwa na tanuru la kuokea Viongozi ili kuendelea kuisaidia Serikali  kushughulika kutatua Changamoto za Wananchi wote"

Pia amewataka Viongozi na wanachama kuendeleza Umoja na Mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa bidiii za kuwasaidia Wananchi kwa kuwa hakuna Chama mbadala cha kuwasemea Wananchi tofauti na CCM na kuwahakikishia Mgombea yeyote atakae pitishwa na CCM atashinda kwa kishindo.

Alisema kuwa anavionea huruma Vyama vya upinzani kwani havitaweza kuwa na Mgombea Mwenye Uwezo wa kushinda  kwani Kazi kubwa inayo fanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John pombe Magufuli kwani inatekeleza Vyema ilani ya CCM katika kipindi cha utendaji wake inaungwa mkono na Wananchi wote wakiwemo wale wa Vyama vya Upinzani.

"Vijana wenzangu Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kushinda kwa haki,Amani na Demokrasia pasina vurugu na Visilani kama inavyofanywa na Vyama Vya Upinzani"

Pia amewataka baadhi ya  Wanachama na Viongozi wa Mkoa wa Arusha kuacha unafiki hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa na kuwataka kusimama na Chama na kutoyumba kwa maslahi ya mtu binafsi

"Ujumbe wangu kwa baadhi ya Viongozi wa Arusha na Wanachama
Kuacha unafiki hasa katika hiki tunachoelekea katika chaguzi za Serikali za mitaa twende tukasimame kwa ajili ya Chama na kutoyumba kwa maslahi ya mtu binafsi"

Aidha Mkuu wa Idara huyo ameshiriki zoezi la Uchangia wa Damu,kutoa mahitaji muhimu kwa Wagonjwa pamoja na Kufanya Usafi katika Hospitali ya West Meru iliyopo Tengeru ,amefungua Tawi jipya Rasmi la Maunt Meru pamoja na kutoa kadi kwa Wanachama wapya 243 walio Jiunga na CCM leo katika Mkutano wa ndani uliofanyika katika wa Patandi.

Katika Ziara hiyo aliambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taiafa Ndg Saitoti Zelote,pamoja na Viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya Mkoa wa Arusha.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: