Thursday, 25 April 2019

Serikali kupandisha vyeo watumishi wa Umma Mei mosi

Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya utumishi na utawala bora George Mkuchika imesema mara baada ya kukamilika kwa upandishaji vyeo watumishi wa umma wapatao 113,520,imewaelekeza waajiri kuendelea na upandishaji vyeo kwa watumishi 193,166 waliokasimiwa katika ikama na Bajeti ya mishahara kwa mwaka 2017/18 kuanzia tarehe 01 Mei 2019.
 
Amesema upandishwaji vyeo kwa watumishi waliokasimiwa katika Ikama na bajeti ya mishahara ya mwaka 2015/16 uliahirishwa Mei 2016 kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi hewa.

Ameelekeza kipaumbele cha kwanza kitolewe kwa utendaji mzuri ambao wanatarajia kustaafu hivi karibuni ili waweze kushughulikiwa mapema iwezekanavyo kabla ya kustaafu

No comments:

Post a comment