Monday, 29 April 2019

Rais Magufuli azindua kiwanda cha Maparachichi


Rais Magufuli amewaahidi wawekezaji wa Kiwanda cha parachichi cha Rungwe kurejesha VAT zinazodaiwa na wawekezaji baada ya uhakiki.

Amesema, Serikali ilizuia kurejesha fedha hizo kutokana na wawekezaji wengi waliwasilisha madeni hewa na hivyo kuisababishia Serikali hasara kubwa.

"Tanzania kwa hewa nadhani tunaongoza, maana kila sehemu ilikuwa ni hewa, lakini na mimi niwaombe wawekezaji hili lenu tutalishughulikia lakini mtuletee madeni yenu halali." alisema JPM.

Aidha Rais Magufuli amemuomba mwekezaji huyo kuwafikiria wakulima kuhusu suala la nyongeza ya bei ya zao lao pamoja na mshahara kwa wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment