Sunday, 14 April 2019

Rais Magufuli Atoa AjIra kwa Vijana 2000 wa JKT

Rais John Magufuli ametoa ajira kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zaidi ya 2,000 walioshiriki ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali.

Vijana hao ni walioshiriki kwenye ujenzi wa nyumba za Serikali, ukuta wa Ikulu ya Chamwino Dodoma, nyumba za magereza pamoja na wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma leo, Rais  Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na kazi kubwa iliyofanywa na vijana hao kwa muda mfupi na gharama nafuu na moyo wa kujitoa kwa ajili ya taifa lao.

Ameelekeza vijana hao waajiriwe katika maeneo mbalimbali ikiwamo jeshini, usalama wa taifa, Takukuru, uhamiaji na taasisi nyingine za Se
rikali

No comments:

Post a comment